Sambaza....


Licha ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Mwadui FC kuhitimisha michezo kumi mfululizo bila ushindi katika ligi kuu Tanzania Bara kocha mkuu wa Mbao FC, Amri Said ‘Stam’ amesema hawezi kukubali ujio wa kocha Ally Bushiri katika timu hiyo na badala yake yupo tayari kuondoka katika timu hiyo ya Mwanza.

Mbao ilishinda kwa mara ya kwanza baada ya kucheza michezo kumi bila ushindi jana Jumatatu katika uwanja wa Kirumba, Mwanza na hivyo kufikisha alama 24. Uongozi wa timu hiyo umemuongeza Bushiri ili asaidiane na Stam kukinoa kikosi hicho cha ‘Wauza Mbao’

Amri Said

“ Nipo tayari kuondoka na kumuachia kocha Bushiri nafasi. Siwezi kufanya kazi na kocha ambaye tunalingana kielemi. Nilitoa mawazo yangu kwa uongozi na nikawaambia kuliko kumleta Bushiri ni heri wamlete Kayuni ( Sunday), au Msolla ( Mshindo) na mimi nipo tayari kuwa msaidizi, ama wamlete kocha mwenye daraja C awe msaidizi wangu lakini wao wamemleta mwalimu ambaye ni daraja B kama mimi, nini ambacho nitajifunza au atajifunza kutoka kwangu?”

“ Nipo tayari kuondoka lakini si kufanya kazi na mwalimu tunayelingana kielemu. Nimewaambia wanilipe stahiki zangu na nipo tayari kumuachia nyumba Bushiri lakini si kufanya kazi pamoja nay eye.” Anasema Amri mlinzi wa zamani wa Simba SC.

Sambaza....