Tetesi

Awesu Awesu huyooo YANGA

Sambaza....

Msimu wa ligi kuu wa mwaka 2019/2020 uliomalizika mwishoni mwa wiki jana  Kagera Sugar ilikuwa ni moja ya timu ambayo ilionesha kiwango na ushindani mkubwa sana kwenye ligi chini ya kocha wao Mecky Mexime.

Mecky Mexime alifanikiwa kuijenga timu ikawa inacheza kitimu zaidi huku baadhi ya wachezaji wakionesha kiwango kikubwa . Baadhi ya wachezaji hao ni kama David Luhende aliyefanikiwa kucheza mechi zote za ligi kuu.

Juma Mhilu mshambuliaji ambaye alitoka Yanga kuja Kagera Sugar na alifanikiwa kung’ara sana kwenye jezi ya Kagera Sugar akifunga magoli zaidi ya 10 kwenye ligi kuu Tanzania bara.

Mchezaji mwingine ambaye alionekana kung’ara hasa kwenye sehemu ya kati ya uwanja ni Awesu Awesu. Tetesi zinadai kuwa mchezaji huyu amefikia makubaliano ya awali na klabu ya Yanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.