CECAFA

Baada ya CAF kuwarudisha, Yanga yaalikwa Kagame

Sambaza....

Jana kulikuwa na habari kubwa sana kwa nchi yetu baada ya shirikisho la soka barani Africa CAF kutupa nafasi nne za uwakilishi katika michuano ya CAF.

Hivo vilabu vinne vitatuwakilisha katika michuano ijayo ya CAF ile ya ligi ya mabingwa barani Afrika na ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Yanga wakishangilia

Simba na Yanga zitatuwakilisha katika michuano ya klabu bingwa Afrika na Azam Fc pamoja na KMC FC watatuwakilisha katika michuano ya kombe la shirikisho.

Baada ya KMC FC na Yanga kuwa kama ingizo jipya, kuna barua nyingine kutoka kwa katibu mkuu wa shirikisho la mpira la Afrika Mashariki na kati (CECAFA) likiwaomba kushiriki michuano ya Kagame.

Michuano hiyo itafanyika katika nchi ya Rwanda ambapo Yanga atakuwa kama timu mwalikwa kwenye michuano hiyo, Tanzania itawakilishwa na timu tatu kwenye michuano hiyo ambazo ni Azam FC kama bingwa mtetezi, Simba na Yanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.