Blog

Baada ya kufuzu, kocha wa Madagascar aula

Sambaza....

Shirikisho la soka la Madagascar, limeongeza mkataba wa kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Nicolas Depuis hadi mwisho wa fainali za mataifa ya Afrika (Afcon)

Depuis, anapata nafasi ya kuiongoza Madagascar kwenye fainali za kwanza kwenye historia ya taifa hilo

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 51, ambaye pia ni sehemu ya watu waliopo kwenye benchi la ufundi la timu ya fluer ya Ufaransa

Mchezo wake wa mwisho wa kuwania kufuzu ni dhidi ya Senegal ambayo pia imefuzu kutoka kwenye kundi lao, pia ameita kikosi cha wachezaji 20

Depuis, amewaita wachezaji Abel Anicet anayecheza nchini Bulgaria, pia golikipa anayecheza nchini Ufaransa ambaye mara yake ya mwisho kuitwa ni mwaka mmoja uliopita

Fainali za Afcon 2019, zinataraji kuanza mapema mwezi Juni nchini Misri


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.