Blog

Harambee Stars itabadilika zaidi vs Stars

Sambaza....

KWA dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mchezo wao wa kwanza wa kundi la tatu dhidi ya Algeria, timu ya Taifa ya Kenya ilionekana kushindwa hata kumiliki mpira kwa dakika moja. Dennis Odhiambo Omino, na nahodha Victor Wanyama walikuwa na wakati mgumu katika eneo la kwanza la kiungo.

Harambe Stars, mazoezini

Katika mfumo wa 4-2-3-1 ambao kocha wa Harambee Stars, Sebastien Migne aliamua kuutumia, viungo washambuliaji watatu- Eric Johana Omondi, Francis Kahata na Ayub Masika walishindwa jukumu walilopewa la kumpasia pasi sahihi mshambulizi pekee, Michael Olunga.

Licha ya kupokea mashambulizi mengi kastika dakika 30 za kwanza, walinzi wa Harambee Stars, Philemon Otieno ( beki wa kulia), Joseph Okumu ( beki wa kati), Musa Mohammed ( beki wa kati) na Aboud Omar ( beki wa kushoto) hawakupoteza umakini licha ya kwamba baadae – dakika ya 31 wakaruhusu penalty ambayo kimsingi ilichangiwa na uwezo mkubwa wa kimbinu wa, Aboud Omarambaye alimlazimisha kiungo wa Kenya, Dennis kumchezea faulo ndani ya eneo la hatari.

Kenya vs Algeria

 

Baghdad Bounedjah alifunga kwa penalty , na baadae dakika nne kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza Riyad Mahrez akafunga goli la pili. Katika soka naweza kusema Kenya imepoteza kutokana na sababu zilezile – siku zote timu bora ambazo hazipewi nafasi zinapokutana na zile zenye kupewa nafasi zikimudu kutoruhusu goli kwa robo saa ya mwisho, hufungwa ndani ya dakika 15’ za mwisho nah ii hutokana na ustahimilivu, uwezo mkubwa wa kimbinu na ufundi kwa wapinzani wao.

UBORA WA KENYA….

Kushindwa kumliki mchezo kwa dakika 45’ za kipindi cha kwanza kuliwafanya Kenya kwenda kujiuliza vizuri na waliporejea kipindi cha pili, yuler Wanyama aliyeonekana kucheza faulo nyingi kipindi cha kwanza akaonyesha tofauti kubwa na Harambee ‘waka-balansi’ mchezo.

Kenya wana uwezo mkubwa wa kubadilika na licha ya muda mwingi wa kipindi cha kwanza kufanya makossa ya mara kwa mara, mabadiliko yao ya haraka kiuzoefu yalivutia kwani ilionekana kila dakika zilivyokuwa zikisonga mbele ndivyo baadhi ya wachezaji walioonyesha uoga mwanzoni wakibadilika na kuonyesha uwezo. Na bahati nyingine nzuri kwao ni kwamba, kocha Sebastien ameonyesha uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo na kuelewa nini cha kufanya.

Olunga hakutengenezewa nafasi yoyote ya wazi dhidi ya Algeria. Attal, Ramy Bensebaini, Djameleddine Benlamri na Aissa Mandi hawakuwa na kazi kubwa lakini bado Harambee Stars walimudu kutengeneza nafasi moja ‘hai’ na nyingine nne za majaribio ambayo hayakuwa na madhara.

Kwa kiwango chao vs ‘Mbwa Mwitu wa Jangwani’ Kenya ni timu itakayokuja tofauti Zaidi katika mchezo ujao dhidi ya Tanzania ambayo wanahifafahamu Zaidi na wamekuwa wakiinyanyasa katika baadhi ya michuano waliyokutana.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x