Ligi Kuu

Hata kwa misimu mitatu, Yanga si Bingwa

Sambaza....

Tazama msimamo huu wa Ligi Kuu  Tanzania bara kuanzia msimu wa 2017/2018 hadi 2019/20. Katika msimamo huu Klabu ya Simba inaongoza kwa kucheza michezo  96, imeshinda michezo 72, kupoteza 7 na Sare 17 ikiwa imejikusanyia jumla ya alama 233. Ikumbukwe katika misimu hiyo mitatu Klabu hii imekuwa kinara wa kufunga magoli, ikiwa imefunga 205 na kufungwa mabao 45 tu.

Kwa upande wa watani zao , Yanga SC wao wanashika nafasi ya pili wakiwa wamecheza mechi 95 , kushinda 55, kutoka sare 24 na kupoteza 16. Alama walizovuna kwa misimu hiyo ni 189 wakifunga mabao 131 na kufungwa mabao 70.

Tazama timu yako ipo nafasi gani hapa

Katika orodha hiyo ni klabu za Azam FC, Prisons Tanzania na Mtibwa Sugar ndizo zipo katika orodha ya timu bora 5 katika mfululizo wa misimu mitatu hadi sasa.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.