John Bocco
Stori

Kiongozi Simba: Sasa njia nyeupe kwa Bocco kuwa kocha

Sambaza....

Mwenyekiti wa Bodi ya klabu ya Simba kwa upande wa mwekezaji Salim Abdallah “Try again” amesema anaona ndoto ya John Bocco ikitimia katika kuwafunza na kuwakuza vijana katika klabu ya Simba.

Salim Abdallah ameyasema hayo leo katika hafla ya kuwatambulisha na kusaini mkataba wa udhamini na kampuni ya masoko ya MobiAd Tanzania.

 

Salim Abdallah “Bocco nahodha wetu na wewe ndoto yako ya kuwa kocha wa vijana inatimia sasa maana mara kwa mara umekuwa ukiniambia kuhusu hilo, hivi karibuni tutaanza ujenzi wa akademi yetu na tayari niliongea na mwekezaji wetu Mohamed Dewji yupo tayari katika hilo.”

Ahmed Alli pia katika hafla hiyo amesema John Bocco aliwahi kumwambia Simba haipaswi kununua mchezaji wa miaka 18 halafu ikawa inasubiri akomae ndio wamtumie.

Ahmed Ally msemaji wa klabu ya Simba Sc.

“Niliwahi kukaa na kapteni Bocco wakati tunatoka Kagera kurudi Mwanza akaniambia Simba haipaswi tena kumnunua mchezaji wa umri mdogo halafu ikasubiri kumkuza akomae ndio imtumie. Maana yake alikua anamaanisha sasa Simba inapaswa kuzalisha vijana wake wenyewe, sasa nadhani ndoto yake imetimia,” alisema Ahmed Alli.

Sambaza....