Kocha Sven Vandebroeck akiwa mazoezini Wydad Casablanca.
Mabingwa Afrika

Kocha Simba Aipeleka Timu Yake Fainali Ligi ya Mabingwa

Sambaza....

Mabingwa watetezi wa Klabu bingwa Afrika Wydad Casablanca wamefanikiwa kutinga fainali tena ya kombe hilo wakiwa chini ya kocha Sven Vandebroek baada ya kuwaondosha Mamelody.

Sven kocha wa zamani wa Simba aliyejiunga na Wydad hivi karibuni amefanikiwa kulinda suluhu aliyoipata katika mchezo wakwanza wakiwa nyumbani na kuwafanikisha Wamorroco hao kwenda fainali kulitetea kombe lao dhidi ya Al Ahly.

Wydad Casablanca na Mamelody Sundowns walikuwa wametoka sare ya 0-0 mjini Casablanca katika mkondo wa kwanza, kabla ya timu zote mbili kutoka sare ya 2-2 nchini Afrika Kusini na Wamorocco hao kushinda kutokana na sheria ya bao la ugenini.

Themba Zwane (katikati) akiwatoka wachezaji wa Wydad Casablanca.

Dakika tano baada ya kipindi cha pili kuanza, Themba Zwane aliifungia Sundowns bao la kuongoza kwa shuti kali nje ya eneo la hatari, kabla ya Ayoub El Amloud kusawazisha dakika ya 72 kwa kichwa kizuri. Dakika saba baadaye, Peter Shalulile aliiweka Sundowns mbele kwa shuti kali alilolipiga ndani ya eneo la hatari hata hivyo, mpira wa kichwa kutoka kwa Mothobi Mvala kwenye wavu wake uliifanya Wydad kusawazisha tena na kutinga fainali.

Kwa upande wa Al Ahly wao wametinga fainali ya CAF Champions League 2023 baada ya kuwafunga Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia kwa jumla ya mabao 4-0. Wakiwa wameshinda mechi ya mkondo wa kwanza kwa raha katika Rades 3-0, Al Ahly waliweza kushinda 1-0 mjini Cairo, shukrani kwa Hussein El-Shahat bao la ushindi kipindi cha kwanza.

Hii itakuwa fainali ya pili mfululizo kwa Wydad na ya tatu dhidi ya Al Ahly, msimu uliopita wawili hao walikutana na Wydad waliibuka washindi kwa na kutwaa kombe hilo. Mechi ya mkondo wa kwanza wa fainali itafanyika Juni 4 mjini Cairo, kabla ya timu zote mbili kukutana tena Juni 11 mjini Casablanca.

Sambaza....