Uhamisho

Kotei na Mkewe waikataa YANGA

Sambaza....

Jana kulikuwa na taarifa za aliyewahi kuwa kiungo wa zamani wa Simba , James Kotei kurejea Tanzania na kujiunga na klabu ya Yanga.

Leo tovuti hii imefuatilia kwa undani sehemu ambayo dili hili limefikia. Tovuti hii imebaini kuwa ni kweli dili hili Lipo na halijafa mpaka sasa hivi.

Vilabu vyote viwili ( Yanga na Kaizer Chiefs ) zimekubaliana kwa pamoja kabisa kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo kuja Yanga.

James Kotei aje Yanga , na Yanga watahusika na kumlipa mshahara kwa kipindi cha miezi sita ya mkopo wake ndani ya Yanga.

Lakini wakala wa James Kotei amedai kuwa ni bora James Kotei auzwe na siyo kutolewa kwa mkopo na Kaizer Chiefs kwenda Yanga.

Kotei (Kushoto)

Kuhusu James Kotei amedai kuwa hawezi kuchezea Yanga kwa sababu ya heshima ambayo  aliiweka ndani ya Simba , Simba na Yanga ni mahasimu wakubwa sana hivi kwa heshima ya mashabiki wa Simba hawezi kuchezea katika klabu ya Yanga.

Kuhusu mke wake ambaye amejifungua hivi karibuni , yeye anaomba wahamie Ghana ili awe karibu na mumewe na malezi ya mwanao.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.