Aishi Manula
Blog

Kwa mara nyingine, Manula ameiangusha Stars

Sambaza kwa marafiki....

HADI kufikia dakika ya 62’ ya mchezo, timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ilikuwa mbele kwa mabao 2-1 dhidi ya ‘majirani zetu’ Kenya ‘Harambee Stars’. Mlinzi wa pembeni, Ochieng Omolo ‘Marcelo’ alifunga goli la kusawazisha la Harambee baada ya kuunganisha mpira wa kona dakika ya 63’.

Wakati mechi ikiendelea kuonekana kuwa wazi mfungaji wa goli la kwanza la Kenya, mshambulizi Michael Olunga alifunga goli la ushindi dakika kumi kabla ya kumalizika kwa mchezo na kuipa timu yake ushindi muhimu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika inayoendelea nchini Misri.

Matokeo ya kipindi cha kwanza

NILITARAJI….

Hata pale Stars ilipopata uongozi wa mchezo kwa mara ya pili dakika ya 43 ( dakika moja baada ya Olunga kusawazisha goli la Saimon Msuva) ambalo lilifungwa dakika ya sita tu ya mchezo nilitaraji kuona Harambee wakifunga angalau magoli matatu katika mchezo wa usiku uliopita.

Olunga alifunga goli la kwanza la Kenya dakika ya 41’ kutokana na muendelezo wa makossa ya golikipa wa Stars, Aishi Manula. Kipa huyo wa Tanzania amekuwa akipigiwa ‘debe’ na kupewa sifa zisizo zake – kama ‘Tanzania One’.

Aishi amekuwa akiokoa baadhi ya nafasi, lakini kuanzia klabuni kwake Simba SC hadi katika timu ya Taifa amekuwa akihusika na magoli mengi ya timu pinzani. Goli la kwanza la Kenya unaweza pia kuwalaumu mabeki, lakini namna kipa huyo alivyoutema mpira ambao baadae ulipigwa ‘tiktak’ na Olunga akiwa katikati ya ‘msitu’ wa wachezaji wa Tanzania.

Aishi Manula akiwa langoni mwa Simba

Goli la pili vilevile, unaweza kuwalaumu walinzi kutokana na kushindwa kuwakaba wachezaji wa Kenya kabla na wakati ulipopigwa mpira wa kona, lakini tazama mpira ule ulipita katika mikono ya Manula na hii inadhihirisha kile nikisemacho mara kwa mara kwamba kipa huyo anakosa mafunzo mazuri.

Mikono ya Aishi haina nguvu, na licha ya timu nzima kushindwa kucheza kitimu sambamba na makossa ya upangaji mbaya wa kikosi kutoka kwa kocha Emmanuel Amunike lakini bado siwezi kuacha kumlaumu Manula kutokana na aina ya magoli ambayo amekuwa akiruhusu katika michezo muhimu.

Stars ina safari ndefu ya kufikia mafanikio katika soka la kimataifa, na michuano hii ya Misri ambayo ni ya pili kihistoria nay a kwanza baada ya kupita miaka 39 inaweza kuwa mwangaza mwingine wa siku za mbele hasa ukizingatia katika michezo miwili wamefanikiwa kufunga magoli mawili.

Wakati Mataifa yenye uzoefu wa michuano kama DR Congo, Afrika Kusini yakitafuta goli lao la kwanza katika michuano, Stars ilishuhudia ikiungana na wenyeji Misri, Ghana, Mali kufunga magoli mawili ndani ya dakika 45’ za kipindi cha kwanza.

Stars inapaswa kuendelea kujifunza , lakini makossa yao katika michuano hii yanapaswa kubebwa na kutazamwa kama njia ya kujikomboa. Vs Kenya, timu haikucheza kitimu, kocha aliipanga na kufanya mabadiliko ya hovyo, Zaidi iliangushwa na kiwango kingine kibovu kutoka kwa Manula.

Aishi ataendelea kusaidia wapinzani kupata magoli hadi lini? Kuanzia Boniphace Maganga, Jean Mundele Makusu na hadi sasa Olunga, Manula ameendelea kuwabeba wapinzani wake licha ya kwanza kwa muda mwingi wa mchezo huokoa hatari nyingi. Kwanini mikono yake haina nguvu?

Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz