Sadala Lipangile "Sadio"
Ligi Kuu

Lipangile: Ndoto ya kila mchezaji kushiriki CHAN!

Sambaza....

Mlinzi wa KMC “Kino Boys” Sadala Lipangile baada ya kua katika wakati mzuri akiwa ànacheza kama mshambuliaji amesema ni ndoto ya kila mchezaji kuvaa jezi na kuitumikia timu ya Taifa “Taifa Stars” kuiwakilisha nchi.

Sadala ameyasema hayo alipokua akiongea na tovuti yako pendwa ilipomtafuta ili kupiga story nae baada ya kuzidi kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika ufungaji. Sadala pia amegusia nafasi yake katika michuano ya CHAN ambayo Tanzania imefuzu kwa mara ya pili baada ya muda mrefu.

Kutokana na kukosekana kwa muendelezo mzuri kwa washambuliaji Wakitanzania wanategemewa kuiwakilisha nchi katika michuano ya CHAN mapema mwaka huu mwezi April, Kandanda ilitaka kujua kama Sadala anaifkiria nafasi hiyo kutokana na uwezo mzuri anaoendelea kuuonyesha katika ufungaji wa magoli katika timu yake ya KMC.

Sadala Lipangile  “Kuhusu timu ya Taifa siwezi sema kama nitaenda au sitoenda kwa maana mwalimu wa timu ya Taifa yeye ndo anafanya uchaguzi  wa wachezaji  ambao wanaokwenda huko (Michuano ya CHAN). Endapo nikichaguliwa nitafurahi kwasababu hii ni ndoto ya kila mchezaji wa Ligi Kuu ambae ni Mtanzania lakini  pia itakua ni hatua nyingine kwenye maisha yangu ya mpira.”

Sadala Lipangile akiwa nahodha akikiongoza kikosi cha KMC dhidi ya Mbao fc.

Sadala pia ameweka wazi nafasi anayoipendelea kucheza akiwa uwanjani na hii ni kutokana na uwezo wa kucheza nafasi mbili kwa ufasaha kabisa. Sadala ana uwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa kati na pia kama mlinzi wa kati huku nafasi zote akizitendea haki.

Lipangile ” napendelea kucheza kama mshambuliaji, ndio “naenjoy”zaidi kandanda niwapo uwanjani.”

Lipangile pia amezungumzia nafasi yake ya sasa akiwa na KMC huku akimuachia mwalimu afanye maamuzi katika kumtumia ili kuweza kuisaidia timu yake.

Sadala “Nitaendelea kucheza kama mshambuliaji lakini siwezi sema nitaacha kucheza nafasi ya ulinzi kwani ikitokea tatizo mwalimu akasema nirudi nyuma kusaidia nitaenda tu kusaidia kama kawaida.”

Mpaka sasa Sadala ameweza kutengeneza nafasi moja ya goli na pia amefunga mabao sita katika michezo mitatu ya hivi karibuni na hivyo kuendelea kuinasua kutoka mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Sambaza....