Blog

Lipuli yagawanyika kuelekea fainali ya Ilulu

Sambaza kwa marafiki....

Klabu ya Lipuli FC yenye makazi yake mjini Iringa imebidi igawanyike makundi mawili ili kuweza kupata matokeo mazuri katika mechi yao muhimu ya fainali kutafuta nafasi ya kucheza michuano ya Kombe la  Shirikisho la Afrika msimu ujao.

Leo, ambayo ni siku ya mwisho ya Ligi kuu, kikosi cha wachezaji wa Lipuli ambao hawakuwahi kutumika katika Ligi Kuu kipo jijini Mbeya kwaajili ya kumaliza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Tanzania Prisons ambao wanahitaji ushindi ili kujihakikishia hawashuki daraja.


…habari inaendelea baada ya tangazo.Wakati huo huo kikosi cha kwanza cha Lipuli kitakuwa njiani leo hii kuelekea Lindi tayari kwa mchezo wao wa fainali muhimu dhidi ya Azam FC ambao leo wapo Dar es salaam kumaliza na timu ya Yanga.

Ratiba ya Fainali ya Azam Sports Confederation Cup imeonekana kutokuwa rafiki sana kwa klabu ya Lipuli kutokana na umbali wa kituo cha fainali. Lakini hata hivyo ingependeza kama fainali hizi zingepewa muda kidogo ili kuzipa nafasi timu kujiandaa baada kumaliza Ligi Kuu.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.