MUNICH, GERMANY - APRIL 25: Arjen Robben of Muenchen gets injured during the UEFA Champions League Semi Final First Leg match between Bayern Muenchen and Real Madrid at the Allianz Arena on April 25, 2018 in Munich, Germany. (Photo by Alexander Hassenstein/Bongarts/Getty Images)
Mabingwa Ulaya

Liverpool kupata ahueni

Sambaza....

Arjen Roben, ataukosa mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Liverpool baada ya kupata majeraha ya mguu

Kiungo Kingsley Koman, anaweza kuwemo kwenye kwa ajili ya mchezo huo utakaofanyika Allianz Arena Jumatano ijayo, ingawa anarejea baada ya kupambana na majeraha ya paja

“Arjen Roben, ni majeruhi na hawezi kuwa sehemu ya kikosi” Kovac aliongea na waandishi wa Habari kabla ya mechi ya ligi ya Ujerumani (Bundesliga) dhidi ya Wolfsburg utakaopigwa Jumamosi

“Coman anarejea natumaini atacheza dhidi ya Liverpool ”

Itakumbukwa katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16, Buyern ililazimisha sale ya 0-0 pale Anfield na inaonekana kutaka kuvifuata vilabu vya Manchester United, FC Porto, Ajax na Tottenham katika kupata nafasi ya kucheza robo fainali

Ajax ilifanya mshtuko wa msimu Jumanne kwa kuifunga Real Madrid 4-1 pale Santiago Bernabeu. Kovac amesema matokeo hayo yamemfanya ahisi kuwataja watu hao wa Eredivise


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.