Blog

Manara namzidi kila kitu mpaka elimu – Antonio Nugaz

Sambaza....

Antonio Nugaz amezidi kujigamba na kujinasibu mbele ya mpinzani wake mkubwa kwa sasa Haji Manara . Watu hawa wawili wamekuwa wakiwa katika ushindani wa maneno kutokana na ufundi wao wote wawili wa kuongea vizuri .

Pia ushindani huu wa maneno umechagizwa kwa kiasi kikubwa na vilabu ambavyo wanafanyia kazi wote wawili. Simba na Yanga ni watani wa jadi , utani wao umekuwa ukiundwa sana na maneno ya utani mara kwa mara.

Antonio Nugaz
Antonio Nugaz (Kulia)

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mchambuzi wa Azam Media , Ally Kamwe alianzisha shindano la kupata msemo upi bora kati ya “Wape Salam” wa Antonio Nugaz na “This Is Simba” wa Haji Manara.

Pamoja na kwamba Antonio Nugaz kudai kuwa msemo wa This Is Simba alianzisha yeye , kwenye shindano hilo Antonio Nugaz alifanikiwa kushinda na msemo wake wa “Wape Salam”.

Haji Manara, Simba Sc

Jana kwenye mazungumzo na Ally Kamwe kupitia mtandao wa Instagram, Ally Kamwe alimuuliza Antonio Nugaz kama anaweza kukutana na Haji Manara na wakawa na mdahalo kati yao wawili mdahalo ambao utahusisha mada ya mpira kwa kuuzungumzia kiundani.

Antonio Nugaz

Antonio Nugaz alitabasamu baada ya kuulizwa swali lile, kisha akajibu kwa kusema swali lile ni jepesi sana kwa sababu anamzidi Haji Manara kwenye vitu vingi kuanzia elimu mpaka mpira wa miguu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.