Sambaza....

Klabu ya Mbeya city fc, imefanya mabadiliko katika benchi lake la ufundi kutokana na uhitaji na nafasi; mabadiliko haya yanahusisha nafasi ya Kocha Msaidizi, Meneja wa Timu na Mtunza vifaa.

Mwalimu Mohamed Kijuso amerejea katika timu yake ya awali (Timu B) na ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo yenye nyota wachanga. Timu hii ya vijana imekua lishe kwa timu kubwa na tuna imani itasaidia kuongeza ushindani katika kikosi chetu. Mwalimu Josiah Steven ambaye ndiye kocha wa magolikipa wa Mbeya City FC anakaimu nafasi ya Kocha msaidizi.

Godfrey Katepa aliyekua meneja wa timu na Rashid Kasiga aliyekua mtunza vifaa wa klabu, wamemaliza mikataba yao na klabu yetu. Klabu itatangaza watumishi watakaochukua nafasi zao.

Sambaza....