Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting

Sambaza....

1 - 2
Mwisho

Mtibwa Sugar FC

Ruvu Shooting

Baada

Timu ya soka ya Ruvu shooting ya Pwani, imepata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa sugar katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliopigwa kunako uwanja wa Manungu Complex uliopo Turiani mjini Morogoro

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani wa aina yake kwa muda wa dakika zote 90, ulishuhudiwa washindi wakitoka nyuma kwa bao 1-0 na hatimaye kuibuka wababe kwenye dakika 45, za kipindi cha pili

Mtibwa sugar ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 38, kupitia kwa Ismaily Aidan, ambapo Ruvu shooting walisawazisha bao hilo dakika chache kabla ya mapumziko kupitia kwa Baraka Mtuwi

Ruvu shooting inayonolewa na kocha Mzanzibar Abdulmutik Haji, ilipata bao lake la pili kunako dakika ya 80, kupitia kwa mshambuliaji wake Issa Kanduru

Kwa matokeo hayo yanaifanya Ruvu shooting, ipande kwa nafasi mbili hadi nafasi ya saba baada ya kufikisha alama 23, ikiwa imecheza michezo 19, huku Mtibwa sugar ikishuka hadi nafasi ya sita ikiwa na alama 27 baada kushuka dimbani mara 19

Na kunako dimba la kumbukumbu ya Sokoine ulishuhudiwa mtanange mwingine wa ligi hiyo, ambao wenyeji Tanzania Prisons waliwaduwaza Mwadui FC baada ya kuwachapa bao 1-0 lililofungwa na Laurian Mpalile kunako dakika ya 50

Matokeo ambayo yanaipeleka Tanzania Prisons hadi nafasi ya tano, ikiwa imejikusanyia jumla ya alama 29, baada ya kucheza michezo 19

Uwanja

Manungu

Taarifa

Tarehe Muda Ligi Msimu Mwisho
19/02/2018 4:00 pm TPL 2017-2018 90'

Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.