Beno Kakolanya
Ligi Kuu

Misimu mitatu, mechi chini ya 20, Beno amejimaliza kuichagua Simba

Sambaza kwa marafiki....

MLINDA mlango Beno Kakolanya amekamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Simba SC kwa mkataba wa miaka miwili. Beno ambaye alitemwa Yanga SC hata kabla ya kumalizika kwa msimu uliopita amesaini Simba na sasa anaingia katika vita ya kuwania nafasi na golikipa namba moja Aishi Manula.

Usajili wa nyanda huyo mwenyeji wa Mbeya ni muendelezo wa ‘kudidimia’ kwake kwa sababu tangu alipotoka Tanzania Prisons ya Mbeya Juni 2016, Beno amecheza michezo isiyozidi 20 tu ya ligi kuu na michuano mingine.

Alijiunga Yanga wakati huo na kuwa golikipa chaguo la tatu nyuma ya Ally Mustapha, Deogratius Munishi n ahata katika msimu wake wa pili ( 2017/18) Beno bado alishindwa kuwa kipa namba moja katika timu ya Yanga licha ya kwamba Deon a Mustapha walikuwa wameondoka.

Kakolanya akisaini Simba Sc

Alishindwa vita ya namba na kipa Mcameroon, Youthe Rostand msimu wa 2017/18 na marta baada ya kupewa kibarua cha kuinoa Yanga kocha Mcongoman, Mwinyi Zahera alimfanya Beno kuwa kipa wake chaguo la kwanza mbele ya Mcongo mwenzake, Klaus Kindoki na chipukizi, Ramadhani Kabwili.

Makosa ya Kindoki katika ushindi wa 4-3 dhidi ya Stand United mwanzoni mwa msimu uliopita yalipita yalimfanya Beno kuwa mbele ya kipa huyo Mcongo ambaye alisainiwa na Zahera huku pia kijana Kabwili akionekana kuhitaji muda Zaidi na kupata uzoefu, Beno akatokea kuwa kipenzi cha Yanga na mara kadhaa kocha Zahera alimkabidhi majukumu ya unahodha.

KUSHINDWA HARAKA….


Baada ya kiwango cha juu katika suluhu-tasa dhidi ya mahasimu wao Simba Oktoba mwaka jana, Beno alijizolea sifa nyingi mno na kwa kweli alistahili sifa hzo kutokana na kazi aliyofanya katika mchezo huo wa raundi ya kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara.

Aliitwa timu ya Taifa kwa mara ya kwanza ndani ya miezi 30 lakini hakupata nafasi yoyote katika michezo dhidi ya Uganda ( Juni, 2018), na ile miwili dhidi ya Cape Verde mwezi Oktoba pia alishindwa kupata nafasi katika game dhidi ya Lesotho mwezi Novemba.

Kakolanya akiwa Taifa Stars

 

Beno hakurejea klabuni kwake Yanga baada ya kutoka Lesotho huku sababu kubwa ikitajwa kudai malimbikizo ya mishahara yake, pesa za usajili, na alipomalizana na uongozi Zaidi ya mwezi mmoja baadae kocha Zahera alimtimua kikosini na licha ya jitihada kubwa kufanywa nma baadhi ya wanachama na waliokuwa viongozi wa muda wa klabu, lakini bado nyada huyo hakutakiwa na kocha mkuu na baadae mkataba wake ukavunjwa kabla ya jana kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa Simba.

AMEFELI?


Bila shaka kwa kipaji alichonacho Beno amefeli sana tangu alipoondoka Prisons misimu mitatu iliyopita. Amecheza michezo michache mno ndani ya miaka mitatu iliyopita na kwa usajili aliokamilisha-kujiunga na Simba ni wazi kipa huyo ataendelea kusubiri nafasi.

Benno akiwa Yanga

Nidhamu yake ndio imepelekea kuondolewa Yanga sehemu ambayo alikuwa na nafasi kubwa ya kufikia malengo yake kimpira, lakini kukubali kwake kuingia katika vita ya namba dhidi ya Aishi ni sawa na kujimaliza Zaidi kimpira licha ya kwamba kimaslai anaweza kuwa amepata kikubwa ndani ya Simba.

Kama atashindwa kuwa kipa chaguo la kwanza Simba msimu ujao itamaanisha kwa misimu mine mfululizo atakuwa si kipa anayecheza michezo ya ligi kuu kwa kiwango cha kutosha. Amecheza michezo chini ya 20 katika misimu mitatu iliyopita na yote hii imetokana na aina ya sajili anazokimbilia.

Wakati anatoka Prisons alikuwa na nafasi kubwa ya kusaini Simba sehem,u ambayo angefanya mambo makubwa lakini akaenda kujimaliza na kukubali kuwa chaguo la tatu nyuma ya Deo na Mustapha katika kikosi cha Yanga na wakati akianza kuaminiwa Yanga akajiingiza katika mzozo uliomtoa kikosini na sasa amekubali kwa mara nyingine kuwa msaidizi wa Aishi ambaye tayari alishinda viya dhidi ya Beno ya kuwa chaguo la kwanza Taifa Stars.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.