Mataifa Afrika

Mwamuzi Tanzania aula AFCON

Sambaza....

Mwamuzi Jonesia Rukyaa ameteuliwa kuwa mwamuzi wa michuano ya vijana ya wanaume wenye umri wa chini ya miaka 17 inayofanyika hapa nchini.

Rukyaa ndiye mwanamke pekee atakayepuliza kipenga katika michuano hiyo, Rukyaa pia aliwahi kuchezesha michuano ya AFCON ya wanawake mwaka jana huenda akapata fursa ya kutangaza zaidi jina lake kwenye michuano ya kombe la dunia la wanawake kule nchini Ufaransa.

Rukyaa ataweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kuchezesha michuano ya kimataifa ya wanaume barani Africa.

Jonesia ndiye mwanamke pekee atakayeshika kipenga kama mwamuzi wa kati, Wanawake wengine ni pamoja Mary Njoroge (Kenya)  Lidwine Rakotozafinoro (Madagascar) ambao wao watakuwa waamuzi wa pembeni wakijumuika na waamuzi wengine 29 walioteuliwa. Waamuzi wote watakwenda kufanya semina kule Casablanca, Morocco kuanzia 31 March hadi kufikia 4 April 2019.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.