Ligi Kuu

NGASSA; Yanga ni ‘klabu ya maisha yangu’ nitasaini muda wowote

Sambaza kwa marafiki....

KIUNGO-mshambulizi Mrisho Khalfan Ngassa anakaribia kuongeza mkataba wa mwaka mmoja Zaidi na klabu yake ya Yanga SC. Ngassa ambaye alifunga magoli saba katika ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita ni kati ya wachezaji ambao mkuu wa benchi la ufundi la klabu bingwa hiyo ya kihostoria nchini, Mwinyi amependekeza kuongezewa kwa mikataba yao.

Ngassa (kulia)

“ Mazungumzo kati ya Ngassa na uongozi yanaenda vizuri na hivi karibuni atasaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kubaki nasi.” Kilisema chanzo cha habari hii kilichoomba hifadhi ya jina lake kutokana na kwamba yeye si msemaji wa klabu hiyo.

Nilifanya jitihada za kumtafuta Ngassa wikendi iliyopita na licha ya kushindwa kuthibitisha ila alishindwa kukataa pia kuhusu kuendelea kuichezea Yanga msimu ujao. “ Nipo kwenye mazungumzo ndiyo na uongozi wangu, naamini hivi karibuni kila kitu kitakuwa sawa na nitaendelea kubaki Yanga . Hii ni klabu ya Maisha yangu”

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.