Mabingwa Afrika

Onyango amkubali pacha wake Inonga asifia kazi yake Uganda

Sambaza....

Kikosi cha Simba juzi kilikua katika Dimba la St Mary’s Entebe Uganda dhidi ya Vipers na kupata ushindi wa bao moja sifuri  na kufufua matumaini yao yakufuzu robo fainali.

Goli pekee la Simba katika mchezo huo lilifungwa na Henock Inonga Baka dakika ya kumi na nane kwa mkwaju wa faulo uliopigwa na Mohamed Hussein.

 

Baada ya kikosi cha Simba kurudi nyumbani jana Jumapili Onyanga anaecheza pacha na Inonga katika eneo la ulinzi wa kati hakusita kumsifia mfunga wa bao na kuonyesha umuhimu wa ushindi huo katika kundi C.

“Ni kitu kizuri sana kwa beki kufunga, hiyo inaonesha kuwa kila mchezaji ni muhimu na bao lake limekuwa muhimu sana kwetu na kwa Wanasimba wote.

Henock Inonga Baka.

Nafikiri sasa tunakwenda kupambana tena kwenye mechi zijazo ili kuona kama tunaweza kwenda mbele zaidi kwenye mashindano haya.” Joash Onyango alisema.

Katika mchezo huo Inonga na Onyango walicheza dakika zote tisini na kufanikiwa kulinda ngome yao na kumaliza mchezo kwa mara ya kwanza bila nyavu zao kutikiswa katika michezo yao ya kundi C ya Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Sambaza....