Blog

Simba ilihitaji kombe tu la Ligi Kuu kuvuna pesa hizi.

Sambaza....

Umewahi waza kuhusu ile sahani uliyoitumia kupiga msosi wako ambao umekupa hicho kitambi au mwili imara?. Sahani hiyo ukishamaliza kuitumi huitamani ukaitupe mbali kwa mafuta mafuta na makando yaliyobakia juu yake. Unaweza kutoithamini lakini ndiyo hiyo inakufanya nadhifu mbele za watu na kupata zaidi yawezekana.

Mara baada ya Simba SC kupewa kombe lake la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara, ikiibuka kinara wa ligi ikiwa na alama ….. tofauti ya alama …. na matani wake Yanga Sc, mambo mengi yaliibuka kuhusu fedha za zawadi atakazo pata na mbali zaidi waliangazia kombe la Ligi Kuu walilopewa.

Kwa upande wa Simba Sc inawezekana ile hatua ya kuchukua kombe tu kwao ilikuwa muhimu sana, yaani kushiba kwanza achilia mbali kuosha vyombo.  Ubingwa huu umempa Simba nafasi tena ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao, nafasi ambayo msimu uliopita waliitumia vizuri zaidi.

Bila kuangalia matumizi ya klabu hii ya Simba Sc na pia bila kuangalia mapato ya mlangoni katika mechi na vyanzo vingine vya klabu kama pango la maduka na ada za wanachama, Simba Sc msimu uliopita imefaidika sana na Ligi Kuu. Hebu tuangalie mapato yao hapa:

Msimu uliopita Simba imekusanya zaidi ya Bilioni Tano (Sio faida kumbuka)

Klabu hii ilitambua umuhimu wa Sahani yake yenye msosi kutoka mwanzo, sahani ambayo baadae imemtunishia tumbo lake zaidi na zaidi na kuonekana wa maana mbele ya jamii. Kila mchezaji anatamani kucheza Simba Sc baada ya matunda haya.

Kumbuka pia ni Simba Sc ambayo mara zote imekuwa ikujaza uwanja wake kwa mechi za Ligi na Kimataifa. Hivyo bado ilitengeneza fedha nyingi katika tiketi za mashabiki.

 

Vilabu vyote 20 vinatakiwa kuiangalia Sahani hii kama ni kitu muhimu, kinachoweza kukupa zaidi katika msimu wake. Timu ikiwa Ligi Kuu tu pekee maanake ina nafasi ya kushiriki mashindano si chini ya matano yaani Ligi ya Mabingwa Afrika, Shirikisho Afrika, FA, Kagame Cup, Mapinduzi Cup au/na Sportpesa Cup. Katika mashindano yote haya licha ya matumizi ila kuna mapato makubwa tu.

Kucheza Ligi Kuu na kupata Kombe ni njia ya kuelekea katika mafanikio mengine, na sasa timu nne zina nafasi ya kula katika sahani kubwa kutoka kwenye Sahani ambayo wengi wetu huona haina maana kwa zawadi na kombe litolewalo.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x