Sambaza....

Klabu ya Wekundu wa Msimbazi  Simba SportsSClub ambao leo wanaanza michuano ya Kimataifa wameanza usajili wao wa dirisha dogo kwa kushusha ndugu yake Didier Drogba.

Simba  imemsajili Zana Oumar Koulibaly kama mlinzi  kulia kutoka katika klabu ya Asec Memosa ili kuziba nafasi ya Shomari Kapombe aliepata majeraha.

Zana Koulibaly mwenye miaka 26 anamudu kucheza kwa ufasaha nafasi ya beki wa kulia anakuja kusaidiana na Shomari Kapombe huku ikimaanisha ndio mwisho wa Nicholas Gyan raia wa Ghana.

Zana Koulibaly ni raia wa Ivory Coast ambae yupo chini ya usimamizi wa Bro Soccer Management ambae pia amepitia katika klabu ya African Sports ya Ivory Coast pia.

 

Sambaza....