Sven Vandebroeck
Mapinduzi Cup

Simba wamekosa kombe la Mapinduzi kwa sababu hizi..

Sambaza....

Sauti ya Shabiki wa Kandanda ni sehemu ambayo hukusanya maoni ya mashabiki kutoka katika mitandao ya kijamii. Haya ni maoni ya shabiki.


Mgalatia Francis J. Lumeya, shabiki wa kandanda, anaangazia kwa maoni yake kile anachoamini kuwa kiliifanya klabu  ya Simba  ishindwe kushinda mchezo wa Jana. Kombe la Mapinduzi ni la kwanza kila mwaka Tanzania.

1. Overconfidence (Kujiamini zaidi)
Simba iliingia uwanjani huku ikiwa inawadharau Mtibwa na kujiona Wana uwezo zaidi. Hili liko wazi sana, wachezaji wa Simba wamekua wakijiona ni mafundi sana kwenye soka hapa bongo na ndio maana wanapata matokeo ambayo hawayataraji, rejea na mechi yao dhidi ya Yanga.

2. Kikosi kilichopangwa
Simba wamepanga kikosi utafikiri wanaenda kucheza na timu ya Mpanda Combine, na hii nayo ni alama ya overconfidence na kujifanya wanakikosi kipana.


Kikosi kilichopangwa hakikua cha kucheza Fainali, Shamte wakumuweka benchi Kapombe, Tairone da Silva wakuanza kwenye mechi kama hii na kumpumzisha wawa kweli? Eti na Rashid Juma naye kaanza pamoja na mgonjwa Miraji Athman halafu mnategemea mshinde?
-Baada ya kuona kikosi cha hicho kukiona, nikajua watapigwa goli hata tatu lakini Mungu si Athumani, Mtibwa nao hawakujiamini…

3. Uhaba wa mbinu kwa Kocha
Tukiri tu, Kocha wa Simba alikosa mbinu kabisa, na hii inaonesha hana uwezo wa kubadilisha matokeo baada ya kufungwa au wakati timu imebanwa. Na kwa style hii, mtafungwa sana otherwise Matola amsaidie sana.

4. Kutokucheza kama timu
Timu ya Simba inacheza utafikiri ni Timu inayokutana kwenye mechi, kila mchezaji anataka aoneshe uwezo wake na anashindwa kuangalia maslahi ya timu.

5. Wachezaji hawana team spirit hawaoneshi kupambana kama inavyokua kwa wapinzani wao, Wana relax as if hawahitaji Magoli…

Kwa mwenendo huu Simba watafungwa sana na wataanza kutafuta mchawi nani wakati wenyewe ndio wahusika.. Mwaka huu wasipokua makini hawapati kikombe hata kimoja, wataishia kuongea tu

Mnajisifia ni Timu kubwa, kubwa kwa umri au uwezo? Kama ni umri sawa ila kwa uwezo ni bado sana ila mnajiaminisha na kujiridhisha kuwa mko vizuri Kumbe hamna kitu….

Hongereni sana Mtibwa, mlistahili ushindi kwa leo, maana mmecheza vizuri kwa kupambana tofauti na wao.


Mgalatia Francis J. Lumeya

Sambaza....