Taifa Stars na Uganda zilipokutana.
AFCON

Stara yafia nyumbani yafifisha matumaini ya kufuzu Afcon

Sambaza....

Mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa huru ya Africa Afcon nchini Ivory Coast umemalizika kwa Timu ya Tanzania ya Taifa kupoteza kwa bao moja kwa sifuri mbele ya Uganda “The Cranes.

Bao la kipindi cha pili la Uganda katika dakika za nyongeza lililofungwa na Rodgers Mato akipokea pasi ya Farook Miya lilitosha kuipa ushindi Uganda na hivyo kufikisha alama nne sawa na Tanzania.

Kwa matokeo hayo sasa timu hizo mbili bado zina nafasi kwa kiasi kikubwa ya kufuzu pamoja na Algeria ambae ndio kinara wa kundi akiwa na alama 12.

Mlinzi wa Tanzania Mohamed Hussein “Tshabalala” akimtoka kiungo wa Uganda.

Algeria tayari wameshafuzu baada ya kupata ushindi dhidi ya Niger na hivyo kufikisha alama 12 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika kundi hilo. Sasa ni wazi ndoto ya Tanzania kufuzu kwa mara ya tatu michuani ya Afcon imeanza kufifia kwani ili Tanzania ifuzu inapaswa kupata ushindi katika michezo miwili iliyobaki.

Michezo miwili iliyobaki ya Tanzania ni ule wa nyumbani unaofwata dhidi ya Niger na wa mwisho ugenini dhidi ya vinara Algeria ambao wameshafuzu.

Katika mchezo huo ulioanza majira ya saa mbili usiku kulitokea hali isiyo ya kawaida baada ya mchezo huo kusimama kwa zaidi ya dakika 20 mwishoni mwa kipindi cha kwanza kutokana na hitilafu ya umeme na hivyo kupelekea baadhi ya taa kushindwa kuwaka vyema.


Sambaza....