Sambaza....

“Nawashukuru na kuwapongeza mashabiki waliofanikisha timu kwenda kwa ndege mkoani Mbeya, hakika Mungu awabariki sana . . hii ndio maana halisi ya timu kumilikiwa na mashabiki wake, sio ajabu kwa mashabiki kuichangia timu yao. . hata Barcelona , Madrid, PSG mashabiki huweka pesa zao ili kufanikisha jambo fulani. Nashangaa hapa nchini jambo limekuwa geni hili.

Objective yetu ni mchezo unaofuata dhidi ya Mbeya City, wachezaji wanatambua umuhimu na ugumu wa mchezo huo! program nzima ya mazoezi niliiacha kwa kocha Mwandila, na alinitaarifu kila hatua waliyofikia nafurahi kuona wametimiza program niliyowaachia, bado michezo miwili (Azam na Mbeya city) tumalize mzunguko wa kwanza na tunahitaji tuwe wa kwanza ili mzunguko wa pili mambo yasiye magumu sana” Mwinyi Zahera mara baada ya kutua JKNIA alfajiri yaeo

Sambaza....