Mataifa Afrika

Abo Rida: Misri itakua tayari kwa michuano

Sambaza....

Mwenyekiti wa kamati ya kuandaa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (Afcon 2019) Hany Abo Rida ameonesha matumaini kuhusu maandalizi ya fainali hizo

Abo Rida, amesema kuwa maandalizi haya ni ya juu sana kwa ajili ya upangaji wa ratiba iliyopangwa kufanyika 12, Aprili 2019 huko Cairo, pia ni ufanisi mzuri wa mashindano yenyewe umefikia pazuri

Misri 2019, itakua Afcon ya kwanza chini ya muundo mpya wa marekebisho wa kujumuisha timu 24, itafanyika 21, Juni hadi 19 Julai 2019

Aidha Abou Rida, alitolea ufafanuzi kuhusu vyombo vya habari vinavyotaraji kuripoti vile vya ndani na vya kimataifa

“Kuhusu tiketi, mchakato utakua mtandaoni ili kuepuka msongano katika vituo vya kuuzia, licha ya muda kua mdogo tunatumia saa nzima kua tayari kwa mechi ya ufunguzi tarehe 21, Juni 2010.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.