Kwenye mechi hii Yanga anaonekana kama kondoo aliyelala
Hapana shaka kesho ni sikukuu ya Simba na Yanga, sikukuu ambayo husimamisha shughuli zote zinazofanyika hapa nchini kwa masaa kadhaa. Mitaa yote hupendezeshwa na bendera za timu hizi mbili, rangi za njano, kijani, nyekundu na nyeupe hutamaraki machoni penu. Hii yote ni kuonesha kuwa timu hizi zinamashabiki wengi kila kona...