Kufuatia kipigo hicho kutoka kwa Raja klabu ya Simba sasa imepata ushindi katika michezo mitatu pekee kwenye kundi lao huku ikifunga mabao kumi na kuruhusu mabao saba.
Mchezo wa kwanza uliopigwa Jijini Dar es salaam Simba walikubali kipigo cha mabao matatu kwa bila mbele ya mashabiki wake na katika mchezo wa leo pia wamekubali kipigo cha mabao matatu kwa moja ugenini katika Jiji la Casablanca.
timu kariba ya Raja Casablanca ni dhahiri inaweza kuonyesha ni kwa kiasi gani kikosi cha Simba kina mapungufu ama kimetimia katika maeneo gani haswa wakiwa nyumbani.
Mashabiki wametambua nguvu yao katika mchezo huu na wametambua kuwa hiki ndo kipindi timu yao inawahitaji zaidi Uwanjani.
Ndo maana wamenunua tiketi kwa wingi tena ndani ya muda mfupi.
Mpaka sasa Simba wana alama tisa nafasi ya pili wakati wapinzani wao Raja wapo kileleni wakiwa na alama 13 hivyo matokeo yoyote hayatobadilisha msimamo wa kundi D.
Kwasasa Shomary hajaitwa kikosini Stars kiasi cha kupelekea wadau wa soka kutoa maoni tofauti na kuwa gumzo baada ya uteuzi huo wa kocha mpya wa Stars Adel Ameorouche.