Mabao ya Simba katika mchezo huo yamepatikana kupitia kwa Emmanuel Okwi na Cletous Chama, na sasa Simba wamekata tiketi ya kucheza nusu fainali na Bandari FC waliowatoa Singida United.
Yanga imeshindwa kwa mara nyingine kuingia hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa Cup baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Kariobangi Sharks ya nchini Kenya.