Ligi Kuu

Huku Haruna kule Chama!

Sambaza....

Kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Simba utakaopigwa March 8 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tayari joto limeshapanda kwa mashabiki na wachezaji wakisubiri kwa hamu mchezo huo.

Hakuna ubishi wa upande wa Yanga chini ya kocha Mbelgiji Luc wameonekana wakijijenga kwa kumtegema Haruna Niyonzima katika eneo la kiungo, huku Mnyarwanda huyo akionekana mtu muhimu kwenye kuinganisha timu kutoka chini akishirikiana na Benard Morrison katika kujenga mashambulizi.

Falsafa ya Simba ni kuweka mpira chini na kuuchezea huku muhimili wa timu ukiwa ni eneo la kiungo. Tangu ujio wa kocha mpya Van Debroeck  Chama amekua mtamu akirudi kucheza kiungo wa kati yaani namna nane huku akitegema muunganiko wake na Jonas Mkude na Francis Kahata.

Haruna Niyonzima akipiga mpira mbele ya nahodha wa Simba Mohamed Hussein.

Akiwa na uwezo mkubwa wa kuchezesha timu akionekana karibu katika eneo la uwanja Haruna Niyonzima amekua kiungo muhimu katika “build up” ya mashambulizi ya Yanga. Amekua akihusika karibu katika shambulizi ambalo Yanga wanalitengeneza.

Sifa ya umiliki mkubwa wa mpira na ufundi mwingi ndio vitu vinavyomtambulisha Haruna. Kwa  kushirikiana na Balama Mapinduzi na Papy Tshishimbi anategemewa kuwa sehemu muhimu ya kuwazima viungo wa Simba wakiongozwa na Chama ili kuutawala mchezo na kuweza kuipa Yanga ushindi.

Haruna Niyonzima akiutenga mpira wa kona.

Ujio wa kocha mpya ambae ni kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Zambia Van Debroek ni kama umemfufua Cleotus Chama kwasasa katika kikosi cha Simba. Chama yule amerudi katika ubora wake na sasa anategemewa kama mpishi mwanzilishi wa mashambulizi ya Simba.

Pasi safi, ubunifu na mikimbio sahihi akiwa na mpira ndivyo vitu ambavyo vinamfanya Chama awe midomoni mwa mashabiki wa Simba. Huku silaha hizo ndizo zinategemewa kuweza kuia Yanga eneo la kiungo na kusiadia Simba kuweza kuutawala mchezo na kupata matokeo.

Cleotus Chama.

Ama kwa hakika ufundi wa viungo hawa wawili wa kigeni kwa kiasi kikubwa unategemewa kunogesha “Derby” ya Kariakoo. Pasi mpenyezo, chenga za maudhi, pasi za mabao na ufundiuwezo wa kumiliki mpira ndivyo vitaamua mchezo wa March 8.

Mchezo huo utatupa majibu ni nani atakaekua mbabe zaidi ya mwenzake katika ufundi na kuisaidia timu yake kutoka  katika eneo la katikati ya uwanja na kuweza kuipa ushindi timu yake siku ya mchezo.

Sambaza....