Blog

Juventus walinunua kwa kazi moja tu- Ronaldo

Sambaza....

Euro milioni 112 zilitumika kumnunua mwanadamu ambaye ana umri wa miaka 34. Ni umri mrefu katika mchezo wa soka, lakini wao hawakusita kumnunua.

Mwanadamu ambaye jana alileta matumaini makubwa ya Juventus kushinda ligi ya mabingwa barani ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996.

Juventus walikuwa nyuma ya magoli 2 walihitaji magoli matatu pekee ili kujihakikishia nafasi ya kuingia hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Na magoli yote matatu yalipatikana kupitia kwa mwanadamu mmoja ambaye ni Cristiano Ronaldo ambaye Juventus walimnunua msimu huu kutoka Realmadrid.

Baada ya mechi hii akizingumza na kituo cha Sky Italia, Cristiano Ronaldo alisema ƙkuwa lengo kuu ya Juventus kumnunua ni yeye kuleta morali kwenye aina ya mechi kama hizi.

Mechi ambazo huonekana ni ngumu na kuna ulazima wa timu kushinda. Mechi ambazo zinahitaji kila mchezaji kuonesha ƙkuwa bado mechi haijaisha.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.