Ligi Kuu

Kandanda yasheherekea na Makambo

Sambaza....

Tovuti yetu ta kandanda.co.tz imeendelea na utaratibu wake wa kusheherekea na wachezaji wa ligi kuu Tanzania bara, ambao wanafunga mabao mengi kwa Mwezi. Mwezi uliopita, Herieter Makambo ndiye aliibuka galacha na kuwa Galacha wa mabao akifungamana na Said Dilunga. Lakini Makambo yeye alifunga mabao muhimu yaliyoisaidia Yanga kukaa kileleni.

Makambo alikabidhiwa zawadi ya kandanda wakati wakifanya mazoezi katika viwanja vya kurasini.

Makambo akiwa na fulana yake ya GALACHA

“Nashukuru sana kwa zawadi hii,  Itaniongezea chachu zaidi, pia nawapongeza kandanda kwa kutambua mchango wangu” Makambo alisema.

Makambo akikabidhiwa fulana ya GALACHA na msimamizi wa tovuti ya kandanda, Thomas Mselemu.

Kwa upande wa meneja wa Yanga bwana Hafidh pia alisema “Nimefurahi kwa mchezaji wangu kupata kitu hiki, ni muhimu kwake na kwa timu. Nadhani hii itamuongezea chachu katika ligi ili aendelee kufunga kila siku na hii itakua na manufaa kwa klabu.”      

Wafungaji mabao mwezi wa 11

Chupa ya zawadi kwaajili ya Makambo, ambayo tovuti ya kandanda hutoa kwa wachezaji kila mwezi.

Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.