Sambaza....

BAADA ya kukosa michezo 11 ya klabu yake kutokana na malazi ya ‘Apendex´, mshambulizi wa Ruvu Shooting, Issa Kanduru amejiunga na wenzake kwa ajili ya maandalizi kuelekea mchezo wao wa Alhamis ijayo dhidi ya Azam FC.

Kanduru ambaye amecheza michezo miwili tu kati ya 13 ya timu yake katika ligi kuu msimu huu anataraji kuwavaa Azam katika uwanja wa Azam Complex akiwa na Said Dilunga mwenye magoli sita hadi sasa.

” Namshukuru Mungu sasa naendelea vizuri na tayari nimeanza mazoezi na wenzangu kuelekea mchezo wetu ujao dhidi ya Azam.” anaanza kusema mchezaji huyo wa zamani wa JKT Mgambo ya Tanga.

” Hadi sasa nimecheza michezo miwili tu, na mchezo mmoja kati ya hiyo nilicheza nikiwa na maumivu. Nilikuwa nikisumbuliwa na matatizo ya pendex.” anaongeza kusema, Kanduru.

Sambaza....