Blog

Kwa Jackson Mayanja, KMC FC ‘imelamba dume’, itapata falsafa yake

Sambaza kwa marafiki....

KATIKA mkutano wake wa kwanza na vyombo vya habari mara baada ya kutambulishwa kuwa kocha mpya wa klabu ya KMC FC, Jackson Mayanja alisema amekuja ‘kuweka alama ya uchezaji’ kwa timu hiyo change katika soka la Tanzania.

Gwiji huyo wa soka la Uganda, amerejea Tanzania alikuwa kwenye kazi kwa miezi minne tu tangu mwaka 2017 alipoondoka Simba SC. Mayanja ambaye aliondoka Simba akiwa msaidizi wa Mcameroon, Joseph Omog kwa sababu zilizotajwa za Kifamilia alirejea katika kazi hiyo Februari mwaka huu alipojiunga na timu ya ligi ya tatu nchini Uganda, Kyetume Football Club.

KMC FC ambayo ilimaliza katika nafasi ya nne katika msimu wake wa kwanza ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita imempoteza aliyekuwa kocha wao mkuu, Etienne Ndayiragije aliyejiunga na wababe wa Afrika Mashariki na Kati, timu ya Azam FC.

Jackson Mayanja

 

Mayanja ambaye hupendelea vikosi vyake kucheza mchezo wa kupasiana na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga anarudi Tanzania akiwa tayari na uzoefu mkubwa kwa sababu amewahi kuifundisha Kagera Sugar FC kwa nyakati mbili tofauti na wababe wa TPL Simba miaka miwili iliyopita.

Licha ya kuweka wazi mipango yake mingi katika klabu hiyo, suala la kuitengenezea falsafa yake kiuchezaji timu ya KMC FC ndilo lililonivutia Zaidi. Kuna umhimu mkubwa kwa klabu kuwa na aina ya mchezo wao utakao watambulisha – mfano, Simba wanapendelea wachezaji wanaoweza mpira nchi na kupasiana, Yanga SC hawajali sana soka la kuvutia, wao wanapendelea nguvu na mchezo wa kukimbiza kwa mipira mirefu.

Mayanja alipokuwa Simba Sc

Itazame Azam FC, licha ya kujiandaa kucheza msimu wa 11 katika ligi kuu Bara, timu hiyo iliyo na uwezo mzuri kiuchumi haina falsafa yoyote ile inayowatambulisha na hili linatokana na mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha. KMC kama wanahitaji kutambulisha falsafa yao kiuchezaji wanapaswa pia kuwa wavumilivu na ninaamini watakuwa hivyo na Mayanja atawapa kitu kizuri.

Kwa hakika uongozi wa timu hiyo umefanya chaguo zuri la kumpa timu yao Mayanja ambaye anakutana na timu yenye mkusanyiko bora wa wachezaji vijana na wale wenye uzoefu. Mayanja hapaswi kupewa ‘target’ katika michuano ya Cecafa Kagame Cup ambayo KMC itashiriki mwezi ujao huko nchini Rwanda, pia inapaswa kuwa hivyo pia katika michuano ya Caf Confederations Cup ambayo wataiwakilisha Tanzania bara kuanzia mwezi Agosti.

Hii ni michuano ya kwanza ya kimataifa kwa timu hiyo inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni, na wakijiandaa na msimu wao wa pili katika ligi kuu bila shaka ‘mtazamo wa klabu na kocha’ utaleta matokeo bora na hili naamini linawezekana kutokana na Mayanja kupata timu ambayo anaweza akapata presha ndiyo, lakini si ile ya kumfanya ashindwe kufikia malengo ya kuitengenezea timu hiyo alama yao ya kiuchezaji hata pale ambapo hatakuwepo.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.