Sambaza....

MSHAMBULIZI wa zamani wa Manyema FC, Polisi Tanzania, Coastal Union, JKT Mgambo na Yanga SC, Malimi Busungu ameamua rasmi kuachana na soka la ushindani.

Busungu ambaye alikuwa akiichezea Lipuli FC tangu msimu uliopita ameuambia mtandao huu Leo Jumanne kuwa ameachana na soka moja kwa moja huku akisita kuweka wazi sababu zilizopelekea kufikia maamuzi hayo.

Mshindi huyo wa mataji mawili ya ligi kuu Tanzania bara kwa sasa yupo kwao Dodoma huku sababu za kimaslai zikisemekana zimechangia kuachana na Lipuli.

” Nimeamua kwa hiari yangu kuachana kabisa na soka.” Anasema, Busungu nilipofanya nae mahojiano mafupi.

” Ni maamuzi tu, siwezi kusema kwa sasa ni nini kimepelekea kufikia uamuzi huu, lakini naomba ieleweke kwamba nimeacha soka moja kwa moja.” Anamaliza kusema mshambulizi huyo aliyekuwa akiwafunga sana Simba SC tangu akiwa Polisi, Mgambo na Yanga.

Sambaza....