EPL

Manchester United watauza sana jezi zao

Sambaza....

Klabu ya Manchester United imezindua jezi zake za msimu wa 2020/21, katika jezi hizo ile ya chaguo la tatu ndiyo imekuwa gumzo kubwa mitandaoni kite duniani. Wakizifananisha na pundamilia na wengine wakihusisha wafungwa. Mtandao wetu unakuletea usiyoyafahamu kuhusu muundo huo wa jezi.

Julia mwisho

Kuna kitu kimoja kuhusu hii jezi. Mchoro wa hii jezi unaitwa Dazzle Camouflage

Dazzle camouflage ni mchoro ambao ulikuwa unatumika kwenye vita vikuu vya kwanza vya dunia.

Dazzle camouflage kwenye meli za Kivita ilikuwa inachorwa kwa kumaanisha hao ni MA – FIGHTER , WANA SPEED , HAWAPIGWI OVYO.

Wenzetu kibiashara kila kitu huwa kina kuwa na theme au meseji ya kibiashara. Meseji ambayo wateja wengi huwa wananunua kwa ajili ya kunimotivate n.k.

Wenzetu hawauzi bidhaa wanauza feelings iliyopo ndani ya bidhaa.

Feelings zinazowekwa kwenye bidhaa ndiyo huwa zinanunuliwa.

Mtu ananunua feeling ya NIKE na siyo kiatu pamoja na kwamba kiatu kinaweza kikawa kizuri lakini ile feelings ya JUST DO IT inanunuliwa sana.

Meli ya kivita

NDIYO maana asilimia kubwa ya Campaigns za Nike ni kuhusu na ujumbe wao wa Just Do It na siyo Campaign za kutangaza mchoro wa kiatu.

Watu wana focus kwenye kuuza na kununua feelings iliyopo ndani ya bidhaa.

Betika Twende Kibingwa

Turudi kwenye hii Dazzle camouflage. Kwanini Nike walifanya vyema kwenye design ya Dazzle camouflage ? kwenye viatu na jezi ya timu moja huko Marekani ?

Walichukua meseji ya Dazzle camouflage ( FIGHTER , SPEED , UNBEATABLE ) afu wakachanga na yao ile ya Just Do It . Wakawezeka kutuambia Just Do It kwa sababu wewe ni fighter , una speed ya kukimbilia mafanikio na uko unbeatable.

Watu wanatumia aspirations na siyo price na uzuri kuuza jezi zao.

Adidas baada ya kuona hivo wakacop design ya dazzle camouflage . Lengo lile lile kuichukua meseji iliyopo kwenye Dazzle Camouflage.

Meseji ambayo ilikuwa inatumika kwenye vita kuu vya kwanza vya dunia.

Meseji hii itafanya kuuza jezi nyie dunia ya tatu mtalalamika kuhusu ubaya wa jezi lakini dunia ya kwanza kwenye soko la Adidas watakuonesha namna ya kuuza feelings za hizi jezi ambazo sisi tunasema ni mbaya.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.