Wachezaji wa Yanga wakishangilia walipoibuka na ushindi wa 2-0 mechi ya Dar es Salaam
Ligi Kuu

Mechi 7 nyumbani, pointi 21, Yanga SC itashinda pia mikoani.

Sambaza....

MABINGWA mara 27 wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC wameendeleza wimbi la ushindi katika uwanja wa Taifa na ushindi wa 1-0 dhidi ya Lipuli FC siku ya jana Jumanne umewafanya kushinda mchezo wao saba mfululizo wakicheza nyumbani.

Licha ya kuendelea kubezwa, kikosi cha kocha Mcongo, Zahera Mwinyi kimeweza kukusanya pointi zote 21 za nyumbani katika michezo yao saba uku wakipata pia alama nne wakicheza ugenini dhidi ya Simba SC na KMC FC. Haya ni matokeo mazuri sana katika ligi kwa timu yoyote ile na Yanga wamepiga hatua nyingi mbele kulinganisha na msimu uliopita.

Ushindi wa michezo saba ya nyumbani ni mtaji wakati watakapoanza safari za nje ya Dar es Salaam mwezi ujao. Msimu uliopita, Yanga waliangushwa zaidi na matokeo yao ya uwanja wa Taifa ambapo walishindwa kuzifunga timu kama Lipuli FC, Mtibwa Sugar FC, Tanzania Prisons, Mwadui FC, Simba, Azam FC.

Mechi zijazo za Yanga (Tarehe hazijabadilishwa bado)

TareheMwenyeji-Mgeni

UGENINI YANGA ITAPETA PIA

Licha ya kuonekana wanashinda kama kwa kubahatisha lakini kiuhalisia Yanga wamefanya vizuri hadi sasa. Pointi 21 walizopata katika michezo yao ya nyumbani ni mwongozo ambao umewafanya waende ugenini wakiwa na matumaini.

Yanga walifanya vizuri msimu uliopita katika michezo yao ya ugenimni na kutokana na ‘ubutu’ wa safu za mashambulizi za timu nyingi za mikoani msimu huu na mbinu anazoendelea kutumia kocha wao Zahera sitashangaa wakipata matokeo hata nje ya Dar es Salaam.

Yanga wanajilinda vizuri na mchezo wao wa Novemba 25 dhidi ya Kagera Sugar FC katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba unaweza kuwapa mwanga zaidi wa nini wanachoweza kupata msimu huu. Msimu uliopita walizifunga timu kama Ndanda FC, Majimajimaji FC, Lipuli FC, Stand United, Kagera Sugar katika game za ugenini lakini kilichokuja kuwaangusha na uwezo wao wa kushinda katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaa.

Naamini, nidhamu, uwezo walio, mbinu na kujitolea kwao kunaweza kuwasaidia isivyotarajiwa kupata matokeo pia katika michezo yao ya ugenini msimu huu. Watu wanaosema Yanga itataabika ugenini wanapaswa pia kujiuliza ni timu gani ambazo tishio.

Tazama, Prisons, Mbeya City FC, Ndanda, Stand, Mwadui, Biashara United, Mbao FC, Alliance School, Mtibwa Sugar, Coastal na hata Singida United zote hizi ni timu zenye mbinu ndogo mno kiufungaji ndiyo maana hadi sasa wanaangaika kufunga magoli ya kutosha. Ukifuatilia michezo mingi msimu huu imemalizika kwa matokeo ya 0-0 hasa ile iliyozihusisha timu hizo nilizozitaja.

Hii ni sababu nyingine ambayo inaweza kuwasukuma Yanga kupata matokeo mazuri katika viwanja vya mikoani. Wana timu nzuri, kocha mzuri, wana uwezo pia kama klabu kubwa kulazimisha matokeo na kama watafanya hivyo wataendelea kushinda hata kule wanakoambiwa hawataweza kufanya hivyo.

Ikumbukwe pia hata kabla ya ligi kuanza wengi walisema, Yanga itayumba lakini matokeo yake imekuwa tofauti na sasa wana nafasi kubwa ya kuongoza ligi kama watashinda kiporo chao dhidi ya Mwadui FC. Wakiendelea kucheza kwa kujituma huku wakisahau mambo yao ya kiuchumi, naona kabisa Yanga ikiendeleza wimbi lao la ushindi hadi mikoani kwa sababu timu nyingi msimu huu zimekumbwa na uhaba wa wafungaji.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x