Kennedy
Uhamisho

Simba yaanza usajili katika na nafasi Wawa.

Sambaza kwa marafiki....

MLINZI wa kati na nahodha wa Singida United, Kennedy Juma anaweza kukamilisha usajili wake wa kujiunga na Simba SC hata kabla ya kuondoka nchini kuelekea Misri ambako ataambatana na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayojiandaa na michuano ya kombe la Mataifa ya Afrika.

Kennedy ambaye amekuwa na misimu miwili ya kuvutia katika kikosi cha Singida amemvutia kocha, Mbelgiji, Patrick Aussems na amempendekeza katika usajili wake mpya kama mbadala wa Salim Mbonde ambaye tayari ameonyeshwa mlango wa kutokea klabuni Simba.

Patrick Aussems, kocha wa Simba Sc

“ Kennedy anaweza kusaini muda wowote kuitumikia Simba, kocha ana mtazama kama mbadala wa muda mrefu katika beki ya kati hasa ukizingatia Mbonde anaondoka, Bukaba (Paul) ana majeraha na Mlipili (Yusuph) bado anapambana kujiweka sawa. “ kilisema chanzo cha habari hii na kuongeza.

“ Ni mlinzi mwenye nguvu na akili ya kupora mipira hivyo kocha anamtazama kama msaada mkubwa katika beki ya kati licha ya kwamba atasajili pia mlinzi mwingine wa kati kutoka nje ya nchi.”

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.