Sambaza....

Zama zinabadilika maendeleo ya tabia nchi na teknolojia mpya zinagusa mifumo ya maisha yetu ya kila siku inashangaza kuona Mgambo bado zana yake ya ulinzi inabaki kuwa KIRUNGU.

Tuachane na hilo, iliichukua Manchester United masaa 12 kuwekana sawa na Molde FK juu ya makubaliano ya kumchukua kwa mkopo Kocha wao hadi mwisho wa msimu huu wa EPL 2018/2019, miezi miwili baada ya ligi yao Noway’s Eliteserien kuanza.

Mkurugenzi mkuu wa Molde FK bwana Neerland anathibitisha kwa kusema ilikuwa surprise kwa wao kupokea ombi hilo baada ya Jose Mourinho kufungashiwa virago kuifundisha timu hiyo, akimaanisha hakukuwa na mawasiliano baina yao na Manchester United kuhusu mpango huo kabla.

Ole

Ujio wa babyfacedassasin  katika viunga vya Carrington umekuwa wenye matarajio chanya sana kwa mtizamo wa wengi hata sisi wa barani Afrika, kwani ndani ya mwezi mmoja tunaiona Manchester united ikionyesha kila ari ya kurudisha hamasa, tija na hali ya kuwa threat kwa yeyote atakayekutana nae.

Tunaona mabeki wa pembeni wakiwa wanacheza on higher up the field ili kuwapa watu wao wa mbele Martial, Rashford na Lingard waingie katika central positions wakati wa kushambulia, huku Pogba akiwa katikati yao kugawa mipira kwa ufasaha na kuendelea kuonyesha uhodari mkubwa wa kupiga pasi ndefu na hili si geni kwani aliwahi kusimulia Ryan Giggs kocha wa timu ya taifa ya Wales kwamba kuna mechi alikuwa anangaalia akiwa na Ole ilikuwa mechi baina ya Manchester United dhidi ya Stoke city, ambayo Manchester united ilishinda Ole alikuwa anamuonyesha jinsi mabeki wa United walivyokuwa wanacheza chini sana ambapo inakuwa ngumu kwa attacking line kufikiwa na mipira kwa wakati na haraka.

Tunaona jinsi alivyomrudisha beki Victor Lindelof katika nafasi yake ya right sided centre-back na kumruhusu kutengeneza nafasi za kumiliki mipira na kuipandisha kutoka nyuma  ambacho kimeongeza ufanisi wake na kuwa katika kiwango bora kabisa ambacho kinamfanya mchambuzi wa masuala ya kabumbu bwana Carragher ambae aliwahi kutamka kuwa Manchester United imepoteza hela kwa kumnunua beki huyo wa kati, kwa sasa yupo katika wakati mgumu kujinasua kwa dhihaka ya maneno kutoka kwa mashabiki.

Tunaona Manchester united ikianzisha mashambulizi kwa haraka, kusambaza mipira kwa haraka kwa kugusa mara chache, watu wa mpira wanapenda kutumia maneno fewer touches na kufanya mashambulizi ya kustukiza mara kadha wa kadha na hii ndio moja ya misingi na miiko ya uchezaji wa Manchester united kama vile unavyoona Baarcelona ama Ajax wakicheza kwa ustadi mkubwa wa kumiliki mpira kwa asilimia kubwa katika mechi zao.

Tunaona mashabiki wa Manchester United wameanza kuwa na morali ya kwenda kuangalia mechi za timu yao viwanjani na sehemu za wazi (bars/pub/lounge)  hali haikuwa hivyo hapo awali kama alivyothibitisha mchambuzi wa masuala ya soka na aliyekuwa nahodha wa Manchester united bwana Gary Neville kwamba kuna baadhi ya mechi za United alikuwa haendi uwanjani kuangalia. Wachambuzi mbali mbali wameanza kutoa mawazo yao kuwaambia mashabiki wasilewe kwa haya matokeo wanayoyapata hivi sasa kwani bado wana safari ndefu kufikia kule wanapopataka yaani kuanza kushinda makombe kama ilivyokuwa huko nyuma ila mimi nipo tofauti nao kidogo kwa kuwaambia wachambuzi wenzangu kuwa mashabiki wana haki hiyo kwa aina ya matokeo mazuri wanayoyapata na uzuri wa mitindo huru na ufundi unaotumika uwanjani kupata matokeo hayo huku kila mchezaji akionyesha kila hali ya kutimilika kwa kiwango chake. Hizi ni ishara tosha za kuelekea kule ambapo walipokuwa awali kuwa timu yenye upinzani na inayoshindania kila kikombe kilicho mbele yao.

Sir Alex Ferguson (Kushhoto) na Ole (Kulia)

Kuwa shabiki wa mpira wa miguu kuna mengi huwa mshabiki anajivunia nayo ukiachana na hili kubwa la kuchukua mataji kwa timu yake, matokeo na jinsi ya uchezaji wa timu yake huwa ni burudani tosha kwao. Kuna timu kama Arsenal ukiangalia uchezaji wao wa kumiliki mpira na Liverpool jinsi wanavyocheza kitimu huwasahaulisha mashabiki wao kama wana muda mrefu hawajashangilia uchukuaji wa vikombe vikubwa barani humo.

Mbinu moja kubwa ambayo mwalimu au kocha akiipatia kuitumia humletea faida kwa 45% ya kupata matokeo chanya ni man management, kubwa kufanya jitihada za dhati na stahiki kwa watendaji wako ili uwavute kwako wakukubali na kuchukulia kufanya nawe kazi kwao sio kazi bali ni fahari. Kizazi hiki cha wachezaji wa sasa ni kizazi cha social media twitter facebook Instagram wachezaji wanafanya yale wanayojisikia kwa wakati huo wakiwa huru hivyo Kocha unahitajika kutokuwa Mwalimu au Kiranja wa nidhamu. Hili Ole amefaulu kwa sasa, amewapa uhuru mkubwa benchi lake la Ufundi ukiwaangalia kina Alvarez Blanco, Carrick, McKenna na fundi mitambo Phelan wanauhusika mkubwa sana kwenye kila maamuzi ya kiufundi yanayotokea katika kila mechi. Ole ameweza kurudisha morali kujiamini na utulivu katika dressing room baina ya wachezaji wake na amekuwa mtulivu sana pale anapojibu suala linamuhusu mchezaji mmoja moja kwa moja. Katika moja ya interviews zake za hivi karibuni aliulizwa swali kuhusu mchezaji Martial kutokuwepo katika kikosi kilichotangazwa kucheza mechi hiyo ya wikendi, aliwajibu waandishi wa habari kuwa mchezaji huyo alipatwa na maradhi ya ghafla hivyo ikapelekea kutokuwa fit kucheza hiyo mechi wakati ukweli wa mambo ndani ya Klabu ni kuwa Martial alichelewa kuripoti kambini hivyo akaadhibiwa.

Kila mshabiki wa mpira wa miguu haswa wa Manchester united ana shauku ya kujua kama Ole atapewa mikoba ya kuwa mwalimu wa kudumu kwa kupewa kandarasi hapo mwisho wa msimu huku wachezaji waliwahi kukipiga katika klabu hiyo wakimpigia chapuo apewe kandarasi ya kudumu mwisho wa msimu  ama wale ambao wanaopamba kurasa za habari za michezo mitandaoni kila siku kina Zidane, Pochettino, Blanc, Jardim, Giggs, Deschamps, Southgate na wengineo wengi wanaotajwa kila kukicha kuja kuwa Kocha wa Manchester united baada ya msimu huu kuisha.

Tuombe uzima muda utakuja kutujuza hili.

Leo nakuacha na swali hili kwako mdau wa kandanda.co.tz, nitajie huyu ni nani?

Alikuwa nahodha wa Manchester united. Alikuwa mkono wa kulia wa Sir Alex pale United, Alikuwepo kipindi Manchester United wanachukua makombe matatu katika msimu mmoja, Ni shabiki wa Manchester united toka akiwa mdogo na ni kipenzi cha kipa David de Gea. Yupo Klabuni hadi sasa anaitumikia Manchester united.

Alikuwa nahodha wa Manchester united, Alikuwa mkono wa kulia wa Sir Alex pale United, Alikuwepo kipindi Manchester United wanachukua makombe matatu katika msimu mmoja, Ni shabiki wa Manchester united toka akiwa mdogo na ni kipenzi cha kipa David de Gea. Yupo Klabuni hadi sasa anaitumikia Manchester united.

Ninamtakia kila la kheri kocha Ole Gunar Solskjaer aka White Masai katika jukumu hili jipya.I

Sambaza....