
Galacha wa Magoli VPL 2019/2020
Mtandao wa Kandanda unarekodi idadi ya magoli yaliyofungwa wakati wa mechi za ligi kuu, Tukiwa na lengo la kusheherekea pamoja na wachezaji wanaoongoza katika ufungwaji magoli kila mwezi na msimu mzima. Msimu wa 2019/2020 Kandanda imeboresha zawadi zaidi baada ya sehemu hii ya zawadi kupewa nguvu na Mgahawa wa Mgahawa Cafe & Restaurant unaopatikana Jijini Dar es Salaam.
Wafungaji bora wa Msimu huu kwa Mwezi
Agosti-Septemba| MK14 | Magoli 6

“Kazi yangu ni kufunga, nahitaji kujitunza na kuelewa hilo. Asante Kandanda kwa kiatu hiki, nitakitunza”
Oktoba |Duma29| Magoli 3

“Hii ni motisha kwangu, nitapambana ‘Hatrick’ zifike hata tano msimu huu”
Novemba |Saliboko10| Magoli 5
“Ninashukuru sana, Kandanda imebuni kitu tofauti sana cha kutuongezea umuhimu wa kufunga
Disemba | Magoli 3
“Pongezi kwenu Kandanda, nashukuru pia kwa kiatu hiki, zawadi zinatupa motisha na hamu ya kufunga zaidi”
Januari | Magoli 4
“Nimefurahi sana kwa hizi zawadi ni kitu kikubwa sana kwangu, nimepata kumbukumbu sahihi kwangu na kwa timu”
Februari| Magoli 5
Kelvin Sabato Kongwe Kagera Sugar FC
Machi |MK 14| Magoli 5
“Nashukuru tena na tena, na kikubwa ni kujiamini na kutambua kazi yangu ”