Makambo
Ligi Kuu

Pale Makambo anapopingana na Dunia.

Sambaza....

Ulimwengu wa mpira umebadilika sana. Umekuwa ulimwengu ambao unatumia sayansi kubwa sana ndani ya mpira.

Ndiyo ulimwengu ambao kila uchwao kuna vitu vingi vipya huongezeka ndani ya mpira. Na ndiyo ulimwengu ambao kila kocha huwaza namna ambavyo anaweza kuwa wa kisasa kwenye mbinu na mfumo.

Ndiyo ulimwengu ambao umemfanya golikipa ambaye anauwezo mkubwa wa kucheza mpira aonekane mwenye thamani kubwa ndani ya soko la mpira.

Makocha wengi wanamtafuta golikipa wa aina hii. Wanamtafuta golikipa ambaye anauwezo mkubwa wa kutumia miguu yake kuliko mikono yake.

Golikipa ambaye anauwezo wa kupiga pasi nyingi ndani ya mchezo mmoja. Golikipa ambaye ataonekana kama mshambuliaji wa kwanza.

Mashambulizi ya timu kuanzia katika eneo lake. Golikipa ambaye anauwezo wa kutoka katika eneo lake na kuja nje ya eneo lake.

Huku ndiko ulimwengu wa mpira ulipo, ndiyo maana leo hii pia makocha wengi hawaangalii kuwa na mabeki wa kati ambayo wanauwezo wa kutumia nguvu sana kukaba.

Kwao wao beki wa kati mwenye uwezo wa kuchezea mpira ana nafasi kubwa sana. Beki wa kati anayepiga sana pasi.

Beki wa kati mwenye uwezo wa kuwa kiungo wa kati. Hawa ndiyo wenye thamani kubwa sana kwenye soko la mpira.

Huwezi kupingana na uhalisia lakini ukweli ndiyo huo. Muda unatupa ukweli ambao hatuupendi. Inawezekana kabisa kina Yashin kwa kipindi wasingekuwa na nafasi mbele ya kina Ederson.

Inawezekana kabisa kina Vidic wasingekuwa na nafasi kubwa mbele ya kina Laporte. Huu ndiyo ukweli wenye uhalisia mgumu kuupokea kabisa.

Ndiyo ukweli ambao unatuonesha kuwa muda huu hata mshambuliaji wa kati anapotea sana kwenye dunia hii ya mpira wa miguu.

Kiumbe hiki kinapotea sana, na watu wanaonekana kabisa kutokuwa na wasiwasi kwa kupotea kwa hawa viumbe.

Na hii ni kwa sababu sayansi ya mpira wa miguu haiwaitaji sana hawa washambuliaji wa kati.

Sayansi ya mpira wa sasa inawategemea wachezaji wanaotoka pembeni mwa uwanja kwa ajili ya kufunga magoli.

Hawa wamekuwa Lulu. Hawa ndiyo wamekuwa wakichukua viatu vya ufungaji bora. Hawa ndiyo wanaotuhamisha kwenda kwenye dunia ambayo hatukuizoea.

Dunia ya wakuwategemea kina Ronaldo De Lima kufunga. Leo hii tunawategemea kina Cristiano Ronaldo, Mohammed Salah kufunga.

Huku ndiko tuliko, huku ndiko tunakoishi. Tumeua vingi sana ambavyo tulizoea kuviona kipindi cha nyuma. Hatuishi tena kwa mazoea ya kipindi cha nyuma.

Wale ma winger wa kukaa pembeni tu muda wote, ma winger teleza hawapo tena siku hizi na hawatakiwi kabisa katika ulimwengu huu wa kisasa wa mpira wa miguu.

Dunia inazunguka na kila inapozunguka lazima ije na mabadiliko ya tabia nchi, ndiyo maana mabadiliko huwezi kuyazuia yanapokuja.

Kuna vitu viwili ambavyo kwenye maisha huwezi kuvizuia. Muda na mabadiliko. Hivi huwezi kuvizuia hata siku moja.

Lakini unaweza kufanya kitu kimoja tu , nacho ni ku-manage muda na mabadiliko , na ndicho kitu ambacho unaweza kukifanya.

Na ndicho kitu ambacho unaweza kukifanya na ukafanikiwa kuishi vizuri tu kipindi ambacho mabadiliko yanapotokea.

Na hiki ndicho Makambo anachokifanya kwa sasa, hajakataa muda huu kuna mabadiliko makubwa kwenye mpira wa miguu.

Muda huu dunia inawakataa sana watu wa aina yake kwenye mpira wa miguu. Vyote hivi hajavikataa ila amejaribu kabisa kuishi kuendana na mabadiliko ya mpira wa miguu.

Anajaribu kuionesha dunia kuwa watu kama wao bado ni lulu. Watu kama wao wanauwezo wa kuendelea kuwepo kama wakitengenezewa mazingira ya kuishi.

Mifumo mingi imekuja kuua uhai ya aina Fulani ya wachezaji dunia. Hatuwaoni tena ma-winger teleza, tunawaona kwa nadra tena washambulijia wa kati.

Na hii ni kwa sababu ya mapinduzi ya kimfumo kwenye mpira. Ndiyo maana kuna wakati unawakumbuka watu aina ya Ronaldo De Lima kila mboni ya jicho inapoingiza taswira ya Makambo.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x