Tetesi

Simba imefagia ‘Mapro’ hawa

Sambaza....

Meza ya Uhamisho ya Kandanda imepokea taarifa kuhusu mabadiliko katika klabu ya Simba  kipindi hiki cha Usajili.  Klabu hiyo inaelekea kuwaacha wachezaji karibia sita wa kimataifa iliyokuwa nao.

Mpaka sasa Simba imeshamuongezea mkataba Meddie Kagere kati ya wachezaji tisa iliyokuwa nao kutoka nje. Katika orodha hiyo ya ‘mapro’ huenda ni Cleatus Chama (CCC) na James Kotei tu wataoungana na Meddie Kagere.

Kagere, Kotei na Chama

Chama, raia kutoka Zambia amekuwa msaada mkubwa sana kwa klabu hiyo wakati wa kampeni ya Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu Tanzania bara. Kwa upande wa Kotei pia ni hivyo hivyo, ameshiriki katika mafanikio ya klabu hiyo vizuri.

Kuna karibia wachezaji wapya nane kutoka nje ambao watatangazwa katika huu utaratibu wao wa Saa Saba Kamili.

Hivi Sasa ni saa Saba Kamili!

Simba kwa sasa inaendelea na utaratibu wake wa kutangaza wachezaji wapya kila ikifika saa saba kamili. Leo pia wapenzi wake wanaendelea kusubiria nani ataongezewa mkataba au nani atasajiliwa.

Wachezaji walioachwa


Pascal Wawa, moja ya mabeki imara katika Ligi Kuu. Amewahi ichezea klabu ya Azam Fc pia.
Zana Coulibaly, mlinzi wa kulia ambaye alisajiliwa kama mbadala wa Shomari Kapombe
Haruna Niyonzima, kiungo msumbufu ambaye alinunuliwa kutoka katika klabu ya Yanga. Hakutumika sana msimu huu, amekuj kutumika mwishoni mwa msimu katika mechi muhimu.
Asante Kwasi, alikuja Simba kisha akapelekwa Lipuli Fc ambako alicheza vizuri. Beki ambaye alikuwa akifunga pia.
Gyan pia hatakuwemo katika msimu ujao wa Ligi Kuu
Juuko Murashid. Beki wa klabu hiyo pia inasemekana yumo katika orodha

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x