Timu hizo zimegawanyika katika makundi mawili yaani kundi A na B. Ambapo washindi wawili (wa kwanza na wapili) kila kundi watapata nafasi ya kufuzu nusu fainali.
Kocha wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) Oscar Mirambo ameushukuru Uongozi wa vyama vya soka ukanda wa Kusini kwa Afrika (COSAFA) kwa kuwaalika kushiriki mashindano ya Vijana ambayo Leo yanaingia hatua ya nusu fainali.