Uhamisho

Upepo’ umebadili mwelekeo, Kahata anaitaka Yanga SC

Sambaza....

INAWEZEKANA Simba SC ilikuwa mstali wa mbele katika mbio za kumuwania kiungo-mchezesha timu Francis Kahata, lakini mara baada ya taarifa za Tanzania Bara kuongezewa timu katika michuano ya Caf- kutoka mbili hadi nne kuanzia msimu ujao, usajili wa Mkenya huyo alinayeelekea kumaliza mkataba wake Gor Mahia FC utaendelea kutikisa.

Katika mazungumzo yangu na mwandishi na mchambuzi mahiri wa soka nchini Kenya ni kwamba, Kahata anaweza kushawishika zaidi kujiunga na Yanga SC na si Simba kama ilivyokuwa ikisema.

” Kahata amekuwa na misimu mitano ya kuvutia Gor, na sasa ni wazi anahitaji kujaribu kutafuta changamoto nyingine nje ya nchi.” anasema mchambuzi huyo wa soka la Kenya.

” Ameshinda kila kitu hapa Kenya na mawazo yake sasa ni kwenda barani ulaya au Afrika Kusini ambako tayari ana ofa kadhaa kutoka klabu za Super Sport United, Kaizer Chiefs na Cape Town City FC. ”

Kagere(kushoto, wakati akiwa Gor mahia) na Kahata (Kulia)

Kenya itashiriki michuano ya Mataifa ya Afrika yanayotarajiwa kuanza mwezi huu huko nchini Misri na Kahata mwenye umri wa miaka 27 yupo kambini nchini Ufaransa akiwa na kikosi cha Harambee Stars.

” Hawezi kufanya maamuzi ya kusaini mahala popote kwa sasa kwa kuwa anaamini anayo nafasi ya kupanmdisha thamani yake katika michuano ya Afcon. ” anaongeza kusema mwandishi huyo wa habari nchini Kenya.

” Hata hapa Kenya kumekuwa taarifa nyingi kuwa anaweza kujiunga na Simba ili kuungana na rafiki yake Kagere ( Meddie) lakini yeye amekuwa akisema mara kadhaa ni shabiki mkubwa wa Yanga, labda anaweza kujiunga na Yanga kama ataamua kuja Tanzania ila ni ngumu kwa sasa kwa sababu anatazama sehemu nyinmgine kwanza.”

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x