Sambaza....

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba SC Jumamosi hii wanakabiliwa na mchezo mgumu wa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Nkana Red Devils huko mjini Kitwe, Zambia.

Licha ya kuiwakilisha nchi katika michuano hiyo ya Caf, Simba wapo katika utetezi wa taji lao la ligi kuu. Kumekuwa na mitazamo tofauti hasa kuhusu ushiriki wa Simba katika michezo ya ligi.

Wakati Azam FC wakiwa tayari wamecheza michezo 15 kati ya 19 ya mzunguko wa kwanza, vinara Yanga SC wakiwa na michezo 14, Simba wamecheza michezo 12 tu na ndiyo timu pekee iliyocheza michezo michache hadi sasa.

Jumatatu hii nilimsikia kocha mkuu wa Yanga, Mcongo, Zahera Mwinyi akilalamika kwa kusema kuwa ´viporo´ vingi vya Simba vinaathiri mwenendo wa ligi. Inawezekana kwa upande fulani, lakini kwa ratiba ya kucheza michezo minne ya Caf ndani ya mwezi mmoja lazima ieleweke michezo ya viporo kwa timu husika ( Simba) haikwepeki.

MISRI, MOROCCO, ALGERIA, AFRIKA KUSINI, ZAMBIA WANASHINDWA PIA

Naweza kutolea ´mfano hai´ kwa Yanga wenyewe wakati wanakimbizana na Simba katika mbio za ubingwa msimu wa 2015/16 wakati walipokuwa wakipambana katika Caf Champions League na baadaye walipofuzu kwa hatua ya makundi ya Caf Confederations Cup.

Yanga mazoezini

Simba walifikia hatua wakagomea kuendelea kucheza michezo yao ya ligi baada ya kuwazidiYanga kwa michezo minne.

Lakini kukumbushia zaidi, mwaka huohuo 2016 Zesco United ya Zambia ilifanifanikiwa kufika nusu fainali ya ligi ya mabingwa Afrika na walipotolewa walirejea katika ligi ya Zambia na kukamilisha michezo yao sita ya kiporo.

Haitoshi, Mamelodi Sundowns yaAfrika Kusini pia walifikia hatua ya fainali na kutwaa ubingwa wa Afrika na katika ligi ya ndani walilazimika kuwekeza viporo visivyopungua mechi tano.

Viporo vya DRC Congo

Nchini Algeria, MO Bejaia iliyokuwa kundi moja na Yanga katika michuano ya kombe la Shirikisho katika ligi ya kwao walikuwa chini kabisa ya msimamo wa ligi kuu Morocco.

Zamalek Sporting Club ya Misri nao walilazimika ´kulimbikiza´ michezo isiyopungua mitano katika ligi kuu Misri kutokana na ushiriki wao katika ligi ya mabingwa Afrika ambako walifika fainali.

Msimamo wa Ligi Misri

2018

Al Ahly Sporting Club ya Misri na Esperance de Tunis ya Tunisia zilifanikiwa kucheza fainali iliyopigwa mwezi uliopita ya Caf Champions League, huku AS Vita Club ya Congo DR na Raja Casablanca ya Morocco zikicheza fainali ya Caf Confederations mwezi huu.

Ukitazama katika ligi zao za ndani timu hizo zote nne utaona zipo nyuma kimichezo na hii inatokana na michezo yao kadhaa kuahirishwa ili kuzipa nafasi ya kujiandaa kikamilifu katika michezo yao ya Caf.

Kama nchi hizi zilizoendelea zaidi kimpira barani Afrika kuliko Tanzania zinashindwa kuepuka michezo ya viporo kwa baadhi ya wawakilishi wao Caf, Tanzania itaweza vipi? Wiki iliyopita, Al Ahly ilikuwa ikiburuza mkia katika ligi kuu ya Misri kutokana na kucheza michezo 7 t- michezo sita pungufu ya viongozi wa ligi hiyo Zamalek.

VIPORO VYA SIMBA NI FAIDA KWA YANGA, AZAM FC

Miaka miwili iliyopita Zesco ilishindwa kutetea ubingwa wao wa ligi kutokana na kucheza nusu fainali ya michuano ya Caf. Wapinzani wao Zanaco FC walikuwa tayari wamemaliza michezo yao na walikuwa mbele kwa alama kati ya 18 dhidi ya Zesco.

Katika michezo yao saba ya kiporo, Zesco United walikuwa na pointi 21 na hizi wangezipata kama tu wangeshinda michezo yote. Wakiwa nyuma kwa alama 18 nyuma ya viongozi wa ligi Zanaco FC ambao tayari walikuwa wamemaliza michezo yao, Zesco walilazimika kuongeza umakini mkubwa katika kila dakika tisini.

Wakashinda mfululizo michezo mitano, wakaanguka katika mchezo wa sita na hapo ikawa furaha kwa Zanaco kwani tayari walijiona mabingwa kwa maana hata kama Zesco wangeshinda mechi yao ya mwisho wangefungana pointi na Zanaco walikuwa na mtaji mkubwa wa tofauti ya magoli.

Mwaka juzi Simba walipoteza nafasi ya kuwa mabingwa wa ligi kuu Bara kutokana na kugoma kuendelea kucheza michezo yao eti hadi Yanga wamalizie viporo vyao. Simba walikuwa moto na walikuwa wakishinda kila mchezo.

Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Ligi Kuu 2018-2019

PosTimuPWDLFAGDPts
138296377156293
238275656272986
3382112554213375
4381316940251555
538148163634250
6381213133240-849
738139163839-148
8381115123242-1048
9381212142537-1248
10381114132935-647
11381211153443-947
12381113143031-146
13381113143039-946
14381112153035-545
15381112153543-845
16381112152741-1445
1738128184752-544
18381014143343-1044
1938128183850-1244
2038411232354-3123
2100000000
2200000000
2300000000
2400000000

Yanga walikuwa nyuma kwa alama nane namichezo mitatu pungufu. Wakashinda kwa taabu 2-1, 2-1, 1-2 dhidi yaJKT Mgambo, Mwadui FC katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Kirumba, Mwanza.

Kutokana na presha ya kufahamu kuangusha alarm yoyote wangeipa Simba nafasi ya kuongoza ligi- michezo yote mitatu walicheza kwa presha kubwa na yote walitangulia kufungwa.

Kwa sasa Yanga wanashinda mechi zao- jambo muhimu zaidi kwao, wamewaacha Simba kwa alama 14- pointi nyingi mno na licha ya Simba kuwa nyuma kwa michezo miwili zaidi yao wanapaswa kuendelea kucheza kwani wapo katika ´umbo ´linalowatisha wapinzani wao.

Wafanye kama Zanaco watashinda ubingwa. Viporo vya Simba ni faida kubwa kwao hasa jama wataendelea kushinda michezo yao.

Sambaza....