Iniesta atuma salamu za kheri kwa swahiba wake.
Kiungo wa timu ya Vissel Kobe ya Japan Andres Iniesta amemshukuru na kumtakia kheri mchezaji Xavier Hernández Creus ‘Xavi’ ambaye ametangaza kustaafu kucheza soka la kulipwa mwishoni mwa msimu huu. Iniesta ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa anajivunia kukua na kucheza pamoja na kiungo Xavi katika timu ya Taifa...