Kuhusu Sisi

Tovuti ya Kandanda.co.tz ilianzishwa mwaka 2010, ikiwa kama ‘blog’ ikiwa na lengo la kukusanya habari za mpira wa miguu na kuziwasilisha kwa wasomaji wake,  Mei 1, 2011 ikaanza rasmi kama tovuti kamili. Tovuti ipo chini ya GALACHA Co. LTD (2014) Namba ya Kampuni 113207 namba ya TIN 136-449-125, pia tunaleseni ya kutoa huduma ya maudhui ya kimtandao kutoka Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) unaweza pitia Sera yetu ya Faragha na Masharti ya Matumizi.

Lugha kuu ya tovuti imekuwa ni Kiswahili, na wakati mwingine imewahi kuwa na mfumo wa lugha mbili, Kiingereza na Kiswahili.


Wasemavyo wasomaji wetu….

“..sema Kandanda nimtandao uko very professional (kitaalamu sana) sema tu wabongo.”

Cet Njovu, Mtaalamu wa IT na Shabiki wa Azam Fc na Man Utd (28/03/2019)
Soma zaidi..


Kwa muda wote huu mpaka sasa tovuti imebaki kuwa na nia moja tu ya kukusanya taarifa zote zinazohusiana na mpira wa miguu, na kuziwasilisha kwa wasomaji wetu kutoka katika vyanzo rasmi kieweledi na kwa mujibu wa sheria za nchi.

Lengo kuu muda wote ni tovuti kuwa sehemu ya habari zote zinazohusiana na mpira wa miguu Tanzania na Duniani, ikiwa pamoja na uchambuzi, matokeo, utabiri, ratiba, msimamo, video na picha, bila kusahau matukio yote yanayohusiana.

Kuwafikia wasomaji wetu katika njia zote ni moja kati ya madhumuni yetu pia , hii ikiwa na maana kuwafikia wanaosoma kupitia Simu, Komputa, App na hapo baadae katika machapisho.

Waandishi wetu wanawasilisha uchambuzi na mawazo yao katika soka la Tanzania na Nje unaweza kuwa sio msimamo wa tovuti, lakini msimamo rasmi wa tovuti utakuwa katika sehemu ya Tahariri.

Kwa maelezo zaidi au Malalamiko kuhusu makala au uandishi wetu, usisite kuwasiliana nasi kupitia anuani hii:

habari@kandanda.co.tz Kwa matangazo bofya hapa


TIMU YETU


 Nafasi  Jina
Msimamizi: Thomas Mselemu
Mhariri:  
Graphics Design:
Mitandao ya Kijamii:
Mpiga picha/Mchambuzi: Sekwao Mwenda
Mwandishi: Thomas Mselemu
Mchambuzi: Abdallah Saleh*
Mchambuzi: Martin Kiyumbi
Mchambuzi: Issack John
Mchambuzi: Baraka Mbolembole*
*Hawaandiki kwa sasa

Unaguswa na uandishi wetu?

Loading ... Loading ...