Mwandishi na Mchambuzi mkongwe na aliyebobea katika familia ya kandanda. Baraka anandika habari na uchambuzi wenye tafakari na jicho la tatu ndani yake. Ukimuelewa utapata ‘madini’ mazuri kutoka kwake, kwake yeye ‘spedi’ ni ‘spedi’ na ‘kijiko’ ni ‘kijiko’.
MABINGWA mara 27 wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania bara, Yanga SC kwa mara ya pili mfululizo wanashinda mechi ambayo hadi wakati wa mapumziko walikuwa nyuma. Jumatatu iliyopita kikosi hicho cha koch Mcongo, Zahera Mwinyi kilipambana ´kufa na kupona´na kutumia robo saa ya mwisho ya mchezo kurudisha goli la Tanzania...
MPENDE mshambulizi huyu, lakini unaruhusiwa kutompenda. Kwa magoli yake saba katika michezo 12 ya ligi kuu Tanzania Bara aliyofanikiwa kuichezea Yanga SC, hakika mashabiki wa klabu yake wanajivunia kuwa na straika huyu lakini kwa wale wanaoangukia upande mwingine kiushabiki wanaweza kuendelea kumpinga lakini ukweli katika ligi ya msimu huu hadi...
KWA misimu miwili ndani ya Yanga SC, golikipa Beno Kakolanya ameanza kikosi cha kwanza katika michezo isiyozidi 25 kati ya 73 ya ligi kuu Tanzania Bara, amecheza chini ya mechi tano kati ya 22 ambazo Yanga wamechezakatika michuano yaCaf ( Champions league + Confederations), na hajawahi hata mara moja kuichezea...
MLINDA mlango wa Mtibwa Sugar FC, Shaaban Kado amesema kikosi chao kinaweza kufika mbali zaidi katika michuano ya Caf Confederations Cup msimu huu. Mtibwa iliichapa 4-0 Northern Dynamo ya Shelisheli katika mchezo wa hatua ya awali kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi jijini Dar es Salaam Jumanne iliyopita. Mabingwa hao...
MEDDIE Kagere alifunga goli lake la 12 tangu aliposainiwa Simba SC Julai iliyopita. Alifungamagoli manne na kuisaidia Simba kufika fainali ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, tayari amefunga magoli saba katika ligi kuu Tanzania Bara, na goli lake la 12 dhidi ya Mbabane Swallows FC jana jioni katika ligi...
Wako wapi, Abuu Ubwa na Haruna Chanongo? Kwanini Said Ndemla bado anaendelea kuchezea Simba SC wakati iliripotiwa alifuzu majaribio yake huko Sweden mwanzoni mwa mwaka huu? Nini kinaendelea kumfanya Thomas Ulimwengu aendelee ‘kutangatanga’ kimpira tangu alipolazimisha kuondoka TP Mazembe Septemba 2016? Maswali yote haya najiuliza na ninayo majibu ya msingi,...
KAMA kocha Mbelgiji, Patrick Aussems ataamua kumchezesha rasmi Jonas Mkude katika nafasi ya kiungo mlinzi na kumuanzisha nje Mghana, James Kotei katika mchezo wao wa Jumatano hii dhidi ya Mbabane Swallows FC, Simba SC haitapata matokeo katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika umri wa miaka 27 Mkude anapaswa...
Mwaka2005 vijana-wapenda soka mtaa wa Area Six-NaneNane, Morogoro tuliamua kuiingiza katika ligi rasmi timu ya mtaani kwetu. Kulikuwa na vijana zaidi ya 35 wenye vipaji vya soka. Na kati yao tulikuwa wawili tu waliokuwa tukicheza nje ya mtaani kwetu kila msimu wa ligi ya TFF ( ligi daraja la nne-...
NAHODHA wa mabingwa mara mbili wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania Bara- Mtibwa Sugar FC, Shaaban Nditti amewaonyawachezaji wenzake nakuwataka kuhakikisha wanaongezaumakini kama timu ili kuwaondoa Northern Dynamo FC katika raundi ya awali ya michuano ya Caf Confederations Cup. Mtibwa inarejea katika michuano ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu...