Pia Injinia Hersi ameonyesha kuheshimu na kuwashukuru viongozi wenzake klabuni hapo kutokana na kazi nzuri na yakutukuka waliyoifanya katika idara zao.
Alli Kamwe amewaambia wapenzi na mashabiki wote wa klabu ya Yanga kila mmoja ana jukumu la kuisaidia Yanga ipate matoekea mazuri na si tu uongozi ama benchi la ufundi ndio wana hilo jukumu.
Kamwe pia amesema kwa sasa hivi wao wanakwenda kuingia katika mchezo huo bila kuifikiria Simba kwani wana wachezaji wakubwa ambao wanajua nini wafanye hivyo mchezo huo ni kama maandalizi ya mchezo wao wa robo fainali.
Endapo Yanga itapata ushindi katika mchezo huo wamwisho kwa wastani mzuri basi watamaliza vinara wa kundi mbele ya US Monastir ambae yeye anamaliza na kibonde Real Bamako.
kubwa zaidi ni tiketi 100 kutoka kwa muunganilo wa Online Media Fc timu hii ya mpira wa miguu ambayo inahusisha wafanyakazi wa media zote za online nchi hii.