Mabingwa Afrika

Yanga Yahamia Chamanzi Kimataifa, Yawaita Mashabiki

Sambaza....

Uongozi wa klabu ya Yanga rasmi umetangaza watatumia uwanja wa Azam Complex uliopo Chamanzi katika mchezo wao wa Ligi ya mabingwa Afrika.

Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari msemaji wa klabu ya Yanga Alli Kamwe alisema “Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha Wanahabari na mashabiki wetu wote wanaotufatilia Mubashara kupitia Azam TV na leo nimekuja kuwapa taarifa za mashindano ya kimataifa na hali ya Kikosi chetu baada ya mechi ya fainali Ngao Jamii,” na kuongeza;

 

“Tutacheza mchezo wetu wa kwanza hatua ya awali wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya ASAS Djibouti kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi tarehe 20.08.2023 majira ya saa 11:00 jioni.”

Katika mkutano huo pia Afisa habari huyo alitaja viingilio vitakavyotumika huku pia akiwaita mashabiki wa klabu yake ya Yanga kuwavaa Wadjibout hao.

Alli Kamwe.

“Viingilio vya mchezo wetu wa kwanza, Jumapili dhidi ya ASAS Djibouti kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi ni, VIP A – tsh 30,000, VIP B – tsh 20,000 na mzunguko – tsh 5,000.

Na kuanzia sasa tiketi zimeshaanza kuuzwa makao makuu ya Klabu Jangwani na tutatangaza vituo vingine kupitia mitandao yetu ya kijamii,” alimalizia Kamwe.

Sambaza....